Jamii ya watu weusi nchini Marekani imelaani hukumu iliyotolewa na jopo
la majaji kuhusu kesi ya mauaji dhidi ya George Zimmerman. Zimmerman
alikuwa anakabiliwa na mashtaka ya kumuua Trayvon Martin, Mmarekani
mweusi mwenye umri wa miaka 17. Jopo hilo la majaji limetoa uamuzi huo
leo ambapo limesema Zimmerman hana hatia na kwamba uchunguzi unaonyesha
hakuhusika na mauaji hayo.
Wazazi wa Travyon wamesema
wanamuachia Mungu hayo yote na kusisitiza kwamba hawajaridhishwa na
uamuzi huo. Wamarekani weusi wamesema uamuzi wa jopo hilo unairudisha
nchi katika zama za ubaguzi wa rangi na wameitaka mahakama ya juu zaidi
ya Marekani kuingilia kati suala hilo.
Maandamano yameripotiwa katika maeneo kadhaa ya Francisco huku
waandamanaji wakibeba mabango yenye ujumbe wa kulaani uamuzi huo. Baadhi
ya mabango yalikuwa na maandishi yanayosema: "Mfumo mzima ni wa
kibaguzi" "Wananchi tunasema Zimmerman ni muuaji"
CHANZO: IRIB
Jamii ya watu weusi nchini Marekani imelaani hukumu iliyotolewa na jopo la majaji kuhusu kesi ya mauaji dhidi ya George Zimmerman. Zimmerman alikuwa anakabiliwa na mashtaka ya kumuua Trayvon Martin, Mmarekani mweusi mwenye umri wa miaka 17. Jopo hilo la majaji limetoa uamuzi huo leo ambapo limesema Zimmerman hana hatia na kwamba uchunguzi unaonyesha hakuhusika na mauaji hayo.
Wazazi wa Travyon wamesema wanamuachia Mungu hayo yote na kusisitiza kwamba hawajaridhishwa na uamuzi huo. Wamarekani weusi wamesema uamuzi wa jopo hilo unairudisha nchi katika zama za ubaguzi wa rangi na wameitaka mahakama ya juu zaidi ya Marekani kuingilia kati suala hilo.
Maandamano yameripotiwa katika maeneo kadhaa ya Francisco huku waandamanaji wakibeba mabango yenye ujumbe wa kulaani uamuzi huo. Baadhi ya mabango yalikuwa na maandishi yanayosema: "Mfumo mzima ni wa kibaguzi" "Wananchi tunasema Zimmerman ni muuaji"
CHANZO: IRIB
إرسال تعليق