Miaka
ya karibuni tumeshuhudia jinsi biashara ya mabenki ilivyopata upinzani
mkubwa baada ya mitandao ya simu kuanza kutoa huduma za kibenki kupitia
simu za mikononi kiasi ambacho mtu anauwezo wa kutembea bila cash lakini
pesa ikiwa kwenye akaunti yake ya simu.
Teknolojia inazidi kurahisisha huduma hiyo, sasa Kampuni ya Uniqul ya
Finland imezindua kile ilichokiita mfumo wa kwanza kuwahi kutokea wa
malipo kwa utambuzi wa SURA ya mteja ‘the first ever payment platform
based on facial recognition’ kama ilivyoripotiwa na Dail Mail.
Kwa teknolojia hii mteja haitaji kutembea na wallet mfukoni wala kadi
ya benki wala simu kwaajili ya kulipia bidhaa dukani, kinachohitajika
wakati wa kufanya shopping ni kamera inawekwa sehemu ya kufanyia malipo
(checkout) ambayo itakuwa inachukua picha ya mteja anayekuwa anataka
kulipia bidhaa zake.

Baada ya picha kuchukuliwa mashine hiyo inafanya kazi ya kuscan
katika database yake ili kuoanisha sura na taarifa za akaunti ya mteja
kisha kukata kiasi anachopaswa kulipa na kupewa risiti na kuondoka,
shughuli hiyo ya malipo kwa mfumo huo inaweza kufanyika kwa sekunde
tano tu.

Kuhusu swala la usalama wa mfumo huo wabunifu wa teknolojia hiyo wa
Uniqul wamedai kuwa teknolojia hiyo ni salama sababau inalindwa na
‘military grade algorithms’ na kuwa inauwezo wa kutambua hata tofauti
ndogo za mapacha.
Msemaji wa kampuni hiyo alisema “In the background our algorithms are processing your biometrical data to find your account in our database as you are approaching the cashier. The whole transaction will be done in less than 5 seconds – the time it usually takes you to pull out your wallet”.
Msemaji wa kampuni hiyo alisema “In the background our algorithms are processing your biometrical data to find your account in our database as you are approaching the cashier. The whole transaction will be done in less than 5 seconds – the time it usually takes you to pull out your wallet”.
Teknolojia hii sio kwamba ni mawazo kwani tayari mfumo huo umeanza
kutumika katika hatua za majaribio huko Finland ambapo usajili wa watu
umeshaanza katika jiji la Helsinki, ili kuweza kuitumia huduma hiyo ni
lazima mtu asajiliwe na kuingia katika system.
Jinsi ya kutumia mfumo huo wateja wanatakiwa kusajili ‘credit cards’ zao ili kuziunganisha na akaunti ya Uniqul.

إرسال تعليق