Janjaro kuja na ujio mpya wa kiutuuzima na ‘Serebuka’

559163_511737735519299_1685950307_n
Msanii wa lebo ya Watanashati Entertainment Dogo Janja anatarajia kuachia ngoma yake ya kwanza ‘Serebuka’ baada maisha ya shule, ambayo anadai ni tofauti na zile alizokuwa anafanya kwaajili ya kuwaburudisha wanafunzi.
Rapper huyo wa Arusha amefanya wimbo huo katika studio za NoizMekah production chini ya producer DX na amewashirikisha Jambo Squad. Anasema hiyo itakuwa ngoma yake ya kwanza rasmi baada ya zile alizokuwa katika maisha ya shule. Amesema itatoka baada tu ya mwezi wa ramadhani kumalizika.
“Nina ngoma yangu ambayo natarajia kuitoa baada ya maisha skonga kwasababu nilikuwa natoa nyimbo kwaajili ya wanafunzi, hazikuwa official songs zangu, zilikuwa kama zawadi kwa wanafunzi,” ameiambia Hisia
“So now nakuja na ‘Serebuka’ nimefanya NoizeMekah Production chini ya producer DX ni ngoma ambayo naamini itaniweka sehemu fulani katika muziki. Natarajia hii ngoma itatoka baada ya mwezi wa ramadhani kumalizika,naomba support wadau wangu.”

Post a Comment

أحدث أقدم