Jeshi huru la Syria FSA limeomba msaada wa silaha toka jumuiya ya kimataifa ili liweze kukabiliana vyema na wapiganaji wenye uhusiano na kundi la kigaidi duniani la al-Qaeda, ombi hilo limekuja siku moja baada ya kuuawa kwa viongozi wa juu wa FSA.
Mauaji hayo yametajwa kuongeza hofu katika jeshi hilo ambalo
inasemekana huenda likaambulia patupu kama halitapatiwa msaada zaidi
kwani Rais Assad emeendelea kuungwa mkono na baadhi ya makundi ya
wapiganaji wa nje ya Syria wanaokinzana na sera za kimagharibi.
Wanaharakati na watetezi wa haki za binadamu waliopo nchini humo
wameafiru kuwa kundi la Hezbollah la nchini Lebanoni limeendelea
kupambana na waasi wanaopingana na Rais Assad.
Wakati hayo yakijiri, mashambulizi makali yameendelea kushuhudiwa katika
mji wa Homs kati ya vikosi vya serikali Rais Bashar a-Assad na
wapinzani kwa zaidi ya majuma mawili sasa.
Shirika la msalaba mwekundi limetoa wito kwa pande zote kuruhusu misaada
ya kibinadamu kuwafikia wahanga wa mapigano katika eneo hilo.
VIA/RFI
Post a Comment