
Mh Pinda amepokea shehena hiyo katika bandari ya Dar es Salaam ambapo amesema inashangaza kuona baadhi ya watu kwa makusudi kabisa wanapotosha ukweli wa mambo kuhusu mradi huo.
Awali wakizungumza kuhusu mradi huo waziri wa nishati na madini Mh
profesa Sospeter Muhongo amesema sasa serikali imeanza safari ya
maendeleo wakati mkurugenzi mtendaji wa shirika la maendeleo ya petrol
nchini TPDC Bw Yona Kilagane amesema hiyo ni awamu ya kwanza ila
zinakuja jumla ya meli 12 zenye shehena hiyo.
Kwa upande wa balozi wa China hapa nchini Dk Lu Youging ambao
ndio wajenzi wa mradi huo wamesema wataendeleza mahusiano mema ambao
yamekuwepo kati ya China na Tanzania kwa muda mrefu huku akitolea mfano
ujenzi wa reli ya Tazara.
CREDITS:ITV
Post a Comment