kahaba
mmoja katika mji wa Naivasha, jimboni Rift Valley, Kenya alinusurika
kufa baada ya kupewa kichapo cha mwizi na makahaba wenzake kwa sababu
wamekerwa na kitendo chake cha kuuza ngono kwa bei rahisi na kuwaharibia
soko.
Wenzake
hao wenye hasira walimtwanga kwa mangumi na mateke, wakimshutumu kwa
kutokuwa na ushirikiano na “kuharibu soko” hasa ukizingatia ilikua ni
kipindi cha mwisho wa mwezi, ambapo wateja wamejaa mkwanja na mahitaji
ya kununua ngono yameongezeka.
Wakati wakimpa kichapo, walitaka
kumkeketa (kumtahiri mwanamke) kwa kutumia chupa iliyovunjika “ili iwe
funzo” lakini akaokolewa na walinzi wa usiku (wengi wao ni wateja wake)
kabla hajafanyiwa kitendo hicho.
Msuguano ulianza mwezi uliopita
pale msichana huyo mwenye umbo nyororo na la kuvutia alihamia mitaa hiyo
kitu ambacho kiliwakera makahaba wazoefu hapo maana walimuona kama
tishio kutokana na urembo wake.
Kwa mujibu wa dereva wa bodaboda
anayeitwa Peter, kahaba huyo amekua ni kivutio na anayependwa na wengi
kutokana na uzuri wa umbo lake na rangi nyeupe ya ngozi yake. Zaidi ya
“kupunguza bei,” inadaiwa kuwa kahaba huyo pia anatoa “huduma” kwa
mkopo, kitu ambacho wenzie hawafanyi, hivyo kuzidi kuwaaribia biashara
zaidi.
“Kwa kawaida, bei ni kati ya Ksh 100 mpaka Ksh 500 (kama TZ
Shs 2,000 mpaka 10,000) inategemeana na mteja. Lakini “Brownie” anauza
kwa hata Kshs 50 (TShs 1,000)” alidai Peter.
Idadi ya wateja wake
ilikua kwa wingi na kwa kasi, kitu kilichopelekea wivu na chuki kutoka
kwa makahaba wengine, ndipo walipofikia uamuzi wa kufanya njama za
kupanga kumpa kichapo “ili iwe fundisho.”
Makahaba hao walitekeleza lengo hilo pale walipomzingira kwenye kona, gizani akiwa peke yake, na kumshambulia kikatili.
“Kwani
unafikiria sisi tutakula wapi kama utaendelea kujiuza hii bei hasara.”
Mmoja wa wanawake hao alimkaripia kwa sauti ya juu.
Kahaba huyo
alipiga mayowe na kuomba msamaha kutoka kwa wanawake hao wenye hasira
wakati anashambuliwa, ndipo walinzi waliposikia na kukimbilia kumuokoa.
Walinzi hao walipofika, walikaripiwa na makahaba hao wakiambiwa kuwa hiyo ni ishu ya wanawake, na wao haiwahusu.
““Unajua
huyu mama huwa ananipatia kwa mkopo siku ninazokuwa nimechacha hivyo
siwezi muacha auliwe na hawa mikora” alisema mmoja wa walinzi hao wakati
wakijaribu kumuokoa mwanamke huyo.
“Wateja” wake wengine wakaingilia kumuokoa kahaba huyo ambaye alikua ameumizwa vibaya, na kumkimbiza hospitali.
Inaonekana
makahaba wazoefu maeneo hayo wanatawala “ngome” yao na lazima wakatiwe
panga na makahaba wapya, ambao lazima wajitambulishe kabla ya kujiunga
kwenye “soko” lao.
“Brownie” bado yuko hospitali akipatiwa matibabu huku wateja wake wakimsubiri apone, ili waendelee kupata “huduma” zake kwa bei nafuu, na kwa mkopo.
“Maisha imekuwa ngumu sana na bei ya kila kitu, hata ya hawa wasichana imepanda sana. Tunaomba serikali iingilie kati ,” mmoja wa walinzi hao alilalamika.
“Brownie” bado yuko hospitali akipatiwa matibabu huku wateja wake wakimsubiri apone, ili waendelee kupata “huduma” zake kwa bei nafuu, na kwa mkopo.
“Maisha imekuwa ngumu sana na bei ya kila kitu, hata ya hawa wasichana imepanda sana. Tunaomba serikali iingilie kati ,” mmoja wa walinzi hao alilalamika.
إرسال تعليق