Kampuni ya AAT yawatunza waandishi wa habari kwa mchango wao juu ya mafunzo ya waendesha pikipiki na bajaj.


Clear_Blue_Acrylic_Trophy_Award_634592631939067572_3

Na Jennifer Chamil-Maelezo.
Taasisi ya Automobile Association Tanzania (AAT) imetoa tuzo kwa waandishi wa habari kutoka katika  vyombo mbalimbali vya habari walio shiriki katika kutoa habari kwa wananchi kuhusu mafunzo yalio tolewa kwa waendesha bajaji na pikipiki  2,500 kuhusu matumizi salama ya barabara.
Tuzo hizo zimetolewa pamoja na fedha taslimu na Rais wa taasisi hiyo Bw. Nizar Jivan katika sherehe fupi iliyofanyika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) jijini Dar es Salaam.
Rais  huyo ametoa tuzo hizo kwa waandishi na watu waliosaidia kukamilisha mafunzo hayo, ambapo    miongoni mwao ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Bw. Assa Mwambene, ambaye tuzo yake ilikabidhiwa kwa Mkurugenzi Msaidizi wa Idara hiy, Zamaradi  Kawawa.
Wengine waliopata tuzo hizo ni Mohamed Ugassa kutoka gazeti la The Guardian, Freginia Ole Swai kutoka ITV, Fred Mwanjara wa Channel Ten, Elias Shamt wa TBC, Miguel Suleiman wa Citizen, Nasongelya Kilyanga wa Daily News, Khadija Mussa wa gazeti la Uhuru, Zainabu Malongo kutoka Mwananchi, Hadja Hamis kutoka Mtanzania, Abas Yusuph mwandishi wa kujitegemea, Judica Benedict wa The Guardian.
Akizungumza na waandishi wa habari katika sherehe hiyo Bw.Nizar amesema kuwa, anawashukuru waandishi wa habari kwa kusaidia kutoa habari kwa wananchi juu ya mafunzo hayo yalio husisha matumizi salama ya barabara na jinsi ya kuepusha ajali za barabarani.
Vilevile taasisi hiyo imeitaka Serikali kuweka mikakati madhubuti ambayo itarahisisha kupambana na matumizi mabaya ya barabara.

Post a Comment

Previous Post Next Post