Na Jennifer Chamil-Maelezo.
Taasisi
ya Automobile Association Tanzania (AAT) imetoa tuzo kwa waandishi wa
habari kutoka katika vyombo mbalimbali vya habari walio shiriki katika
kutoa habari kwa wananchi kuhusu mafunzo yalio tolewa kwa waendesha
bajaji na pikipiki 2,500 kuhusu matumizi salama ya barabara.
Tuzo
hizo zimetolewa pamoja na fedha taslimu na Rais wa taasisi hiyo Bw.
Nizar Jivan katika sherehe fupi iliyofanyika ukumbi wa Idara ya Habari
(MAELEZO) jijini Dar es Salaam.
Rais
huyo ametoa tuzo hizo kwa waandishi na watu waliosaidia kukamilisha
mafunzo hayo, ambapo miongoni mwao ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari
Maelezo Bw. Assa Mwambene, ambaye tuzo yake ilikabidhiwa kwa Mkurugenzi
Msaidizi wa Idara hiy, Zamaradi Kawawa.
Wengine
waliopata tuzo hizo ni Mohamed Ugassa kutoka gazeti la The Guardian,
Freginia Ole Swai kutoka ITV, Fred Mwanjara wa Channel Ten, Elias Shamt
wa TBC, Miguel Suleiman wa Citizen, Nasongelya Kilyanga wa Daily News,
Khadija Mussa wa gazeti la Uhuru, Zainabu Malongo kutoka Mwananchi,
Hadja Hamis kutoka Mtanzania, Abas Yusuph mwandishi wa kujitegemea,
Judica Benedict wa The Guardian.
Akizungumza
na waandishi wa habari katika sherehe hiyo Bw.Nizar amesema kuwa,
anawashukuru waandishi wa habari kwa kusaidia kutoa habari kwa wananchi
juu ya mafunzo hayo yalio husisha matumizi salama ya barabara na jinsi
ya kuepusha ajali za barabarani.
Vilevile taasisi hiyo imeitaka Serikali kuweka mikakati madhubuti ambayo itarahisisha kupambana na matumizi mabaya ya barabara.
إرسال تعليق