Wiki
hii moja ya vitu vilivyozua mijadala mikubwa nchini Kenya ni pamoja na
muswaada wa sheria ya ndoa ‘Marriage Bill 2013’ iliyowasilishwa katika
bunge la Kenya Jumanne (July 16) ambayo pamoja na mambo mengine, unasema
adhabu ya kifungo cha miaka 5 na fidia ya million 1 ya Kenya (zaidi ya
m 18TSH) kwa mwanaume/mwanamke atakayetoa ahadi za ndoa na kushindwa
kuzitimiza kwa mujibu wa mtandao wa Niaje.
Haya ni baadhi ya mapendekezo yaliyomo katika muswaada huo wa sheria ya ndoa 2013 kwa mujibu wa mtandao wa Ghalfa:
1.Wapenzi ambao wataahidiana ndoa na baadaye mmoja kushindwa
kutimiza ahadi hiyo atatakiwa kulipa fidia endapo sheria hiyo
itapitishwa.
2.Muswaada huo unatoa nafasi kwa wapenzi kusajili ndoa yao kama ‘monogamous’ inayoruhusu wanandoa kuwa na mume/mke mmoja tu.
3.Endapo mwanaume akitaka kuongeza mke/wake wengine ni lazima
mke/wake zake waidhinishe maamuzi hayo, mwanaume ambaye ataoa wake zaidi
kwa siri anaweza kushitakiwa
4. Wanandoa watakuwa na haki sawa juu ya mali za ndoa, endapo
wanandoa watakubaliana mwanaume aoe wake wengine, haki za mali za ndoa
kwa mke wa kwanza zitalindwa.
Muswaada huu umepokelewa kwa hisia tofauti na wakenya ambao wengi wao
hususani wanaume wameonesha kutoridhishwa kwa madai kuwa imependelea
zaidi upande mmoja wa wanawake

إرسال تعليق