Mama
mzazi wa aliyekuwa muigizaji wa filamu, mchekeshaji na muimbaji,
marehemu Hussein Ramadhani aka Sharo Milionea ameendelea kuingia hofu
juu ya kupotea kwa baadhi ya mali alizoacha mwanae.
Akiongea Kitale ambaye aliyekuwa rafiki yake kipenzi, Kitale amesema
mama yake Sharo ameingiwa na hofu baada ya kuona kimya kutokana na ahadi
alizopewa baada ya matanga na kwamba kuna mali ambazo alitakiwa
kukabidhiwa.
“Mali ambazo aliahidiwa mama Sharo ni gari aina ya Oppa ambayo ina
thamani ya milioni 16 na marehemu Sharo aliazima gari la aina ya Toyota
Harrier ambalo alipatanalo ajali lililokuwa na thamani ya milioni 25 ila
jamaa mwenye Toyota Harrier ile siku ya matanga aliomba akabidhiwe Oppa
aitumie Halafu baadaye atamkabidhi mama Sharo ila kwa bahati mbaya
mpaka leo mama Sharo hajakabidhiwa gari, ndiyo maana yule mama anakuwa
na wasiwasi, sasa baadhi ya watu wanadhani mimi nashikilia hizo mali
wakati ndivyo sivyo,” amesema Kitale.
“Sharo alikuwa anamiliki gari aina ya Oppa na Bajaj, mimi kuna filamu
ya mwisho niliyofanya na marehemu Sharo na kwa makubaliano yetu tukija
kuuza tuweze kugawana mapato kwahiyo watanzania watambue hivyo.”
إرسال تعليق