Nahodha wa Liverpool, Steven Gerrard akiwa amewakumbatia wachezaji wawili wa Thailand baada ya mechi hiyo |
MSHAMBULIAJI Luis Suarez ameendelea
kuitumikia Liverpool kwa shingo upande majira haya ya joto hata katika
mchezo wa leo, ikiibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Thailand, mjini
Bangkok.
Mshambuliaji huyo wa Uruguay, ambaye anataka kuondoka Anfield, aliingia Uwanja Rajamangala dakika 30 za mwisho.
Suarez alikaribia kufunga baada ya kupewa pasi na Steven Gerrard, lakini akakosa.
Mabao ya Liverpool leo yamefungwa na Coutinho dakika ya 17, Aspas dakika ya 49 na Gerrard dakika ya 60.
Kikosi cha Liverpool leo kilikuwa:
Mignolet, Enrique, Agger, Toure/Skrtel dk69, Johnson, Lucas,
Allen/Alberto dk80, Gerrard, Coutinho/Henderson dk69, Aspas/Ibe dk63 na
Borini/Suarez dk63.
Thailand: Hathairattanakool, Butmathan, Sokam, Daosawang, Wannasri, Lasoh, Anan, Songkrasin, Kraisorn, Wongsa na Dangda.
La kwanza: Philippe Coutinho akishangilia bao la kwanza
Gerrard akiurushia busu umati, baada ya kufunga bao la tatu la Liverpool
Coutinho akifunga kwa kuupitisha mpira katikati ya mabeki wa Thailand walioanguka
Hakieleweki: Luis Suarez akiinuka kwenye benchi
anamaambaa
Suarez alipoingia alifanya vitu
إرسال تعليق