LYRICS:- KAMA HUWEZI - BY RAMA DEE Feat LADY JAYDEE



Verse 1: JayDee


Vipi mpenzi huoni mbali

Kweli huwezi kwenda mbali, na mie

Kweli mengi huletwa ndani

Si halali kuyapokea yote unitupie

Tutagombana kila siku mpenzi

Tutaudhiana kila siku ndani

Tutatishana kugawana mali

Bila kumjua mchawi wetu nani


Chorus:

Kama huwezi

Kuwa mkweli

Kamwe mpenzi mbele hatutofika mama

Kama pesa, zipo za kututosha ma X2


Verse 2: Rama Dee


Hizi lawama ziishie leo leo

Isifikie wakwe wanivue vyeo

Kwa gubu lako tu, mamii

Lawama zako zisinitie uchizi

Nibadili mipango yetu mingi

Hatutagombana tukifata yetu

Hatutaudhiana tukipanga yetu

Hatutafikia kugawana mali, mimi na wee


Rudia Chorus x 2


Tutagombana kila siku mpenzi

Tutaudhiana kila siku ndani

Tutatishana kugawana mali

Bila kumjua mchawi wetu nani


Hatutagombana tukifata yetu

Hatutaudhiana tukipanga yetu

Hatutafikia kugawana mali

Mimi na we


Rudia chorus x 2


Song written by Rama Dee


Enjoy

Post a Comment

Previous Post Next Post