
Ndege ya shirika la Asiana,iliyokuwa ikitoka Seoul, kusini mwa Korea,
imeanguka wakati ikitua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa San
Francisco na kuuwa watu wawili, na kujeruhi wengi.
Ndege hiyo iliyokuwa na abiria zaidi ya 300, ilipata ajali hiyo siku ya
jumamosi asubuhi mara baada ya kutua katika njia yake kwa ajili ya
kusima.
Abiria 180 walikimbizwa katika hospitali zilizo karibu huku wengine wakitoka na majeraha madogo madogo.
Kutokana
na maelezo ya maofisa wa shirika hilo la ndege, ajali ya ndege
yaohaijatokana na tatizo la injini bali kuna tatizo lingine ambali bado
halijajulikana kwa sababu hali ya hewa ilikuwa shwari kabisa.
Kwenye
mabaki ya ndege hiyo wataalamu wameweza kupata kifaa kinachoitwa Black
Box ambacho hu-rekodi mambo yote ya safari ya ndege, na hivyo kusaidia
kupata majibu juu ya sababu ya ajali hii.




Post a Comment