Mazishi ya kiongozi wa upinzani aliyeuawa nchini Tunisia,Mohammed Brahmi
REUTERS/Anis Mili |
Polisi nchini Tunisia wamelazimika kutumia mabomu ya kutoa
machozi kuwatawanya maelfu ya waandamnaji katika barabara za mji wa Sidi
Bouzid wanaondamana kutaka serikali ya Kislamu kuondoka madarakani.
Waandamanaji hao wameendelea kupaza sauti zao kwa zaidi ya juma moja
sasa baada ya kuuawa kwa kiongozi wa upinzani Mohammed Brahmi.
Wafanyakazi waliokuwa wanakwenda kazini siku ya jumatatu
walizuiliwa kuingia sehemu zao za kazi na waandamanaji hao waliowataka
kujiunga nao ili kuendelea kushinikiza chama cha Ennahda kuondoka
madarakani.
Wakati makabiliano hayo yakiendelea, viongozi wa serikali wamekuwa
wakikutana kwa dharura kujadili mustakabali wa maandamano hayo ambayo
yanayofiwa huenda yakawa makubwa kama yale yaliyoingusha serikali ya
Rais wa zamani Zine El Abidine Ben Ali.
Mohammed Brahmi anakuwa kiongozi wa pili wa upinzani nchini humo
kuuawa baada ya kiongozi mwingine Chokri Belaid kupigwa risaisi na
kuuawa nyumbani kwake mapema mwaka huu.
Upinzani nchini Tunisia umeendelea kuitumu serikali kwa kuwauawa viongozi wao tuhma ambazo serikali imeendelea kukanusha
إرسال تعليق