Kukiwa
kuna muendelezo wa wasanii wa muziki wa kizazi kipya kupata watoto leo
msanii wa muziki huo Mabeste amesema naye anatarajia kupata mtoto muda
wowote. Amesema mtoto huyo akiwa wa kiume atampa jina, Kendrick na kama
akiwa wa kike atamuita Kelly.
Muda mchache uliopita Mabeste alikuwa maendeo ya Mikocheni akifanya
manunuzi ya maandalizi ya kijacho, ambapo amesema alikuwa ananunua
mapambo ya chumba cha mwanae huyo pamoja na stika kwaajili ya kuta za
chumba atakapokuwa akilala mtoto.
“Kupata mtoto kwetu ni neema kwani nilikaa kwa muda mrefu bila
kuongea na baba yangu lakini baada ya kinachokaribia kuja mabadiliko
yametokea ndio maana tumechagua majina yenye maana kwaajili ya
kijacho,”Mabeste ameongea na kipindi cha XXL

Post a Comment