Majambazi yaliyomjeruhi mwanachuo na kupora UDSM yakamatwa

 
Imeandikwa na Katuma Masamba via HabariLeo

WATUHUMIWA wanne wa ujambazi uliotokea Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kusababisha majeruhi wamekamatwa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Ally Mlege alisema majambazi hao walikamatwa Julai 8, mwaka huu katika eneo la Ubungo kituo cha daladala ambapo askari waliweka mtego wa kuwakamata.

Kamanda Mlege alisema baada ya kukamatwa kwa watuhumiwa hao walipopekuliwa walikutwa na simu na bunduki aina ya Shot Gun ikiwa na risasi moja, kompyuta mpakato mbili Toshiba, simu ya mkononi Samsung C3230, panga pamoja na nyundo.

Alisema baada ya kuhojiwa , inadaiwa walikiri kuhusika na tukio la unyang'anganyi kwa kutumia silaha la Juni 21, mwaka huu katika Bweni la Yombo One na kumjeruhi mwanafunzi huyo kwa risasi tumboni kisha kupora mali mbalimbali.

"Mbali na tukio hilo pia wamekiri kuhusika na matukio ya 

Post a Comment

أحدث أقدم