Makampuni ya biashara kuweni karibu na jamii

Picture
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Evarest Ndikilo akishirikiana na Mfanyakazi wa Vodacom Mwanza Jumao Khamis kukabidhi kitoweo cha mbuzi kwa wanafunzi wa moja ya madrasa za jijini humo zilizonufaika na sadaka ya vyakula kutoka Vodacom Foundation kupitia kampeni ya Pamoja na Vodacom ya kufuturisha na kusaidia madarasa na Makundi mengine ya wasiojiweza wakati wa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.Hafla hiyo ilihusisha pia futari kwa wanafunzi wa madrasa na jumuiya za kiislamu za jijini Mwanza.Kulia ni Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Sheikh Salum Fereji.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarest Ndikilo amesema kuwa kitengo cha kusaidia Jamii cha kampuni ya Vodacom - Vodacom Foundation ni kielelezo cha namna ambavyo makampuni ya biashara nchini yanavyotakiwa kuwa karibu na jamii na kusaidia kutatua changamoto za kijamii nchini.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa huyo wakati wa hafla ya kufuturisha wanafunzi wa Madrasa na wanajumuiya ya Kiislamu wa Mwanza iliyoandaliwa na Vodacom katika viwanja vya Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana jijini humo.

Ndikilo amesema Vodacom Foundation imeonesha mchango mkubwa katika kubadili maisha ya watu na 
ustawi wa jamii hapa nchini kwa mifano ambayo inaonekana wazi na kila mtu.

"Vodacom imekuwa ikifanya kazi kubwa sana katika kusaidia jamii kwa kutambua na kuunga mkono juhudi za serikali, taasisi na vikundi vya kijamii  kwa kuwezesha maendeleo ya kijamii na kubadili maisha ya watu, hili lipo wazi."Alisema Ndikilo.

Aliongeza "Ni kutokana na shabaha yake hiyo Vodacom inaonesha kwa vitendo jinsi ambavyo kampuni ya biashara inavyoweza kuwa karibu na jamii inamofanyia biashara na kutoa ushirikianao katika kutatua changamoto zinazoikabili jamii hizo kw aukubw ana uzito unaostahili," aliongeza Ndikilo.

Ndikilo amesema ingawa ni jambo la kawaida kwa makampuni ya biashara kurudisha faida kwa jamii - CSR lakini kiwango kikubwa cha fedha ambacho Vodacom hutumia kila mwaka kinaonesha utashi na shabaha ya ziada kwa kampuni hiyo eneo hilo la uwajibikaji kwa jamii - CSR.

Mkuu huyo wa Mkoa ametumia pia nafasi hiyo kusifu ubunifu wa Vodacom katika kusaidia jamii ubunifu ambao unaongeza tija katika kila wanachokitoa kwa jamii.

Ndikilo alikuwa akizungumzia utaratibu wa Vodacom katika kufuturisha kupitia mpango wake wa Pamoja na Vodacom ambapo Vodacom hutumia utaratibu w akuwaweka pamoja na pia kutumia nguvu kazi ya wakazi wa eneo husika katika kufanikisha futari hizo ikiwemo uandaazi wa futari.
"Tukio hili linafaida kuu mbili, mosi ni kwamba wenzetu hawa (Vodacom)wanatumia vikundi vya akina mama katika kuandaa shughuli yote, ni wazi kwamba kwa kufanya hivyo wanasaidia kuinua vipato vya akina mama hao na hatiame kuwafungulia fursa za biashara na pili ni jinsi wanavyokusanya kwa pamoja wanafunzi na watu kutoka sehemu mbalimbali na kupata furati kwa pamoja na hivyo kujenga mshikamano."

Amesema Vodacom ingeweza kupeleka kazi hiyo kwa makampuni makubwa ya vyakula ama hoteli lakini wameona ni vema kutumia nafasi hiyo kuchangia vipato vya akina mama.

"Wenzetu hawa wangeweza kulipeleka tukio hili mahali popote lakini hawakufanya hivyo kwa makusudi kabisa ili na wale watu wa chini ambao hawana uwezo wa kupata kazi kubwa kwenye makampuni kunufaika na fursa za kufanya biashara na Vodacom."Aliongeza Mkuu huyo wa Mkoa huku akiwashauri wale wote walionufaika na fursa hiyo kuhakikisha wanatumia kipato wlaichopata kujiendeleza zaidi.

Akizungumzia umuhimu wa hafla za aina hiyo, Mkuu huyo wa Mkoa amesema ni jambo jema ambalo ni sehemu ya Baraka za mwezi mtukufu wa Ramadhan huku akitoa rai kwa viongozi wa dini kutumia kipindi hiki kukemea mabaya na kuhimizana mema ikiwemo Amani, mshikamano na umoja wa kitaifa.

"Nawaomba viongozi wa dini mtumie mikusanyiko ya aina hii kuwekeza neno la Amani kwa waumini wetu na hasa vijana ambao wapo kwenye wakati mgumu wa kushawishiwa kutumika katika kuvuruga Amani ya nchi."
Kwa upande wake Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim amesema kampeni ya Pamoja na Vodacom hulenga kuipatia nafasi kampuni hiyo kuonesha upendo kwa kuheshimu na kuthamini utukufu wa mfungo wa Ramadhani.

"Ni kwa zaidi ya miaka sita sasa utaratibu huu wa kufuturisha umeendelea, ni jambo ambalo Vodacom tunajivunia nalo kuona kwamba tunapata nafasi ya kukaa pamoja na kushiriki futari na wanafunzi wa madrasa na jumuiya za kiislamu hapa nchini.

Mwalim amesema katika mwezi huu mtukufu Vodacom Foundation imetenga Sh 50 Milioni kwa ajili ya kazi ya kufuturisha na kutoa sadaka kwa madrasa mbalimbali hapa nchini.

Post a Comment

Previous Post Next Post