Siri
za wizi uliotokea Makao Makuu ya Polisi mkoani Mwanza zimeanza kuvuja
ambapo imebainika kuwa kompyuta aina ya laptop zilizoibwa ndani ya
chumba cha vielelezo zilikuwa za ushahidi wa kesi ya wezi wa mashine za
kuchukulia fedha(ATM).
Katika
wizi huo wa benki ambao ulifanyika kwenye mashine za ATM mbalimbali na
watuhumiwa watatu kunaswa Februari 10, mwaka huu saa 6 usiku wakiiba
kwenye ATM za NMB,Tawi la PPF Plaza, Polisi walinasa vitu vingi vya
watuhumiwa hao ikiwa ni pamoja na kompyuta mbili ambazo zinadaiwa kuibwa
kituoni hapo juzi.
Habari
zilizopatikana kutoka ndani ya Polisi zimeeleza kwamba katika wizi huo
uliotokea katika maghala ya Polisi, moja kati ya vifaa vilivyoibwa ni
mafaili mbalimbali ya vielelezo kadhaa vya kesi zinazochunguzwa na
polisi ikiwa ni pamoja na laptop hizo ambazo zilikuwa ni ushahidi kwa
kesi hiyo ya wizi wa ATM.
Kamanda wa
Polisi mkoani Mwanza, Ernest Mangu alipoulizwa kuhusiana na vielelezo
vilivyoibwa Polisi, alikanusha kwamba laptop hizo zilikuwa kielelezo cha
kesi za wizi wa fedha katika ATM lakini pia hakuwa tayari kueleza
zilikuwa za kesi gani.
Wakati
Kamanda huyo akikanusha baadhi ya askari ambao wanahusika na uchunguzi
huo wamedai kuwa wizi huo uliendeshwa na maofisa wa polisi wasio
waaminifu na kubainisha hakuna wizi unaoweza kufanywa na watu kutoka nje
ya polisi.
Habari na Frederick Katulanda, Mwananchi
Post a Comment