
MANCHESTER UNITED imeijaribu tena Barcelona juu uhamisho wa kiungo Cesc Fabregas kwa kupeleka ofa mpya ya pauni milioni 30 masaa machache baada David Moyes kufurahia ushindi wake wa kwanza kama kocha wa United.
Lakini mabingwa hao wa ligi kuu sasa watakumbana na ucheleweshaji wa majibu katika kipindi hiki ambacho Barcelona wanasubiri kumtangaza kocha mpya baada Tito Vilanova kuachia ngazi kwa matatizo ya kiafya.
Wiki iliyopita United iliwasilisha ofa ya pauni milioni 26 kwa mchezaji huyo wa zamani wa Arsenal.
Huku timu ikielekea Japan kwa mechi mbili zijazo katika ziara yao ya dunia, Moyes anatarajiwa kugeuzia shingo usajili akizingatia kuwa ofa yake ya pauni milioni 12 kwa Leighton Baines imekataliwa huku kiungo Thiago akijunga na Bayern Munich.
Kuondoka kwa Vilanova Nou Camp kumevuruga mambo kwenye dili la Fabregas ambaye jana alionyesha sapoti yake kwa kocha wake wa zamani kwa kuandika kwenye Twitter: “Afya njema iwe kwako, Tito. Sote tuko pamoja nawe, niko nyuma yako”.
Barcelona haitafanya maamuzi yoyote kuhusu wachezaji hadi hapo atakapotangazwa kocha mpya.
إرسال تعليق