
MASHINDANO
ya kitaifa ya kuhifadhi Quran tukufu yamemalizika jana, huku walemavu
wa viungo wakiwa kivutio cha aina yake, kwa kuonyesha maajabu.
Walioshangiliwa
na hata kuwatoa machozi watazamaji walikuwa ni Ummy Kuluthumu Swaleh
Saidi kutoka Pemba, ambaye hakuwa na miguu wala mikono pamoja na Seif
Salim Said ambaye ni mlemavu wa kuona na kusikia, waliweza kusoma vizuri
bila kubabaika huku wakiwapita hata wale waliokuwa na viungo kamili.
Mashindano
hayo yalimalizika jana Dar es Salaam katika ukumbi wa Diamond Jubilee
ambapo yalihusisha washiriki 72 kutoka Tanzania Bara na
Visiwani.Walemavu hao pamoja na wengine sita, walizawadiwa fedha taslim
pamoja na fimbo za kuwawezesha kutembea.
Nafasi
ya mshindi wa kwanza kwa wavulana ilikwenda kwa Abdul Hamid na msichana
alikuwa Suria Ally Bakari ambao kwa pamoja walipewa Bajaji na fedha
taslim sh. 500,000. Washindi wa mashindano hayo yaliyoandaliwa na Eshe
Sururu Foundation, yaligawanywa katika makundi matano, kwa upande
wanawake na wanaume, huku washindi wengine wakiondoka na pikipiki,
baiskeli, vyereheni na fedha taslim.
Katibu
wa kamati ya maandalizi, Issah Ramadhan Mohamed alisema kuwa madhumuni
ya kuandaa mashindano hayo ni kuibua ari kwa vijana wa kiislam waweze
kusoma Quran Tukufu kwa mustakabali wa maisha mema.
Alisema
yalishirikisha wasichana 38 na wavulana 34 ambapo kila upande alitoka
mshindi wa kwanza hadi wa tatu na yaligawanywa kwa ngazi tano ikiwemo
kuhifadhi Juzuu 20,10, tano na tatu
إرسال تعليق