Mbowe azindua Kanda ya Kusini

Picture
Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe akihutubia wananchi jana katika mkutano wa hadhara wa uzinduzi wa Kanda ya Kusini uliofanyika katika viwanja vya stendi ya malori mjini Songea.
Picha hii na zote zilizopachikwa hapo chini ni kutoka: AzimioLetu.blogspot.com

Na zifuatazo zilikuwa ni Live Updates za mkutano huo kutoka kwa Tumaini Makene na Mohamedi Mtoi via JF.

YANAYOJIRI T2015CDM - 01

Leo (17 Julai 2013) majira ya saa 9, Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, kamanda Freeman Mbowe akiandamana na viongozi kutoka Makao Makuu na wabunge wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, atakuwa na mkutano wa hadhara mjini Songea, Ruvuma, ikiwa ni sehemu ya ukamilishaji wa uzinduzi wa Kanda ya Kusini (Mtwara, Ruvuma na Lindi).

• Mapokezi makubwa (maandamano) yataanzia eneo la Bomba mbili. Mbali ya ku-set agenda za masuala mbalimbali, kisiasa, kijamii na kiuchumi, ambayo CHADEMA inasimamia kwa ajili ya Watanzania, pia atazungumzia masuala kadhaa, zikiwemo kauli za Mzee/Viongozi Wastaafu (ref. Mwananchi ya leo) kuwa wanapaswa kuwa statesmen, hasa katika kushauri taifa kushughulikia primary contradictions kwa ajili ya
 kutatua matatizo yanayoikabili nchi na Watanzania, badala ya (wao) kutumika kufanya propaganda kwa kuzungumzia secondary contradictions (mfano suala la amani linafanyiwa propaganda sana), huku taifa likiangamizwa na CCM.

• Baada ya itifaki kadhaa kukamilika, Sasa hivi ndio msafara unaelekea eneo la mkutano. Wananchi wa Songea hasa wanawake, kama kawaida yao wako pembeni mwa barabara kwa shangwe zenye heri na baraka.

• Kamanda Hashim kutoka Mtwara 'haitoki'. Si gesi tu, rasilimali zote tuhoji,tuachwa vipi, manufaa yetu ni nini?
Ukihoji serikali iliyoshindwa unapigwa, CHADEMA ndiyo dira ya mabadiliko yetu.

• Kamanda Hashimu kutoka Mtwara, anasema, wananchi wa Songea na maeneo mengine waondoe unyonge, Mtwara wameshagangamala, na wao waamke na kuinga mkono CHADEMA

• Ally Chitanda anamjibu Pinda kuwa amedanganywa, tatizo la ununuzi wa korosho mikoa ya Kusini ni matokeo ya kushindwa kwa sera za CCM. Asiwadanganye watu kwa kuunda kamati ya watu watamo (5).

• Ruvuma ndipo mapambano ya kumng'oa mkoloni yalianzia na kumng'oa Kaburu yalikuwa yakiendeshewa hapa. Mkoa huu una historia ya mapambano ya kukomesha udhalimu na manyanyaso -John Mrema.

• Kigaila sasa: ni nyumba ya ajabu. Rais kama baba naye analia, wananchi ktk makundi mbalimbali wanalia, hata polisi pamoja na kupiga mabomu wanalia, mshahara hautoshi.

• Kila mtu ndani ya nchi analia,Watanzania wako hoi, lakini waliopewa dhamana ya kuongoza nao wanalia. Tatizo ni CCM. Sasa tuache kulalamika. Tuchukue hatu. Ndiyo maana tumekuja kuwazindulia kanda. Watu wachukue kadi, pale tulipo waanze kufungua msingi kila kitongoji na kila nyumba kumi, wekeni balozi wa CHADEMA.

• Wakati balozi wa CCM ataandika barua kwa pesa, wa CHADEMA atafanya bure!

• Msigwa. Wajibu namba moja wa serikali yoyote madarakani ni kulinda usalama na uhai wa raia wake. Serikali ya CCM imepoteza uhalaki kwa sababu vyombo vya dola vinatuhumiwa kushiriki vitendo vya mauaji. Ni kwa sababu Ccm haina tena uwezo wa hoja na sera kupambana na CHADEMA. Sasa wanapiga, wanatisha na kuua watu!

• Malcom X anasema "Kama mtu anakuonea, anakupiga kwa kukuonea, kujilinda si vurugu ila ni akili".
 
Viongozi mbalimbali wakitoa salam kwa wananchi wakati katika mkutano wa uzinduzi wa Kanda ya Kusini ya mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma uliofanyika katika viwanja vya Stendi ya Malori mjini Songea
 

Post a Comment

أحدث أقدم