Mchumba wa Nay wa Mitego akipoteza kichanga chake tumboni baada ya kuanguka

df510a9eeb3d11e2971f22000a1f8c25_7
Rapper Nay wa Mitego leo anasherehekea siku ya kuzaliwa ya mchumba wake aliyekuwa mjamzito kwa huzuni kubwa baada ya mchumba wake huyo kukipoteza kichanga chao kufuatia kuanguka jana usiku.
“Jana usiku mke wangu alianguka, alifikia tumbo kwahiyo akawa anasikia kizunguzungu nilipompeleka hospitali daktari akasema mtoto amekufa,” Nay ameiambia Bongo5.
Awali, Nay wa Mitego ameweka picha ya mchumba wake kwenye Instagram akiwa hospitali na kuandika: Happy bday my lv, Mungu akupe maisha marefu na yenye mafanikio tele. Japo imekukuta uko vibaya tumempoteza kijacho bt ni mipango ya mungu, nakupenda sana mke..!! #966# happy bday 2u ma.”

Post a Comment

Previous Post Next Post