Msanii
wa lebo ya Watanashati Entertainment Dogo Janja anatarajia kuachia
ngoma yake ya kwanza ‘Serebuka’ baada maisha ya shule, ambayo anadai ni
tofauti na zile alizokuwa anafanya kwaajili ya kuwaburudisha wanafunzi.
Rapper huyo wa Arusha amefanya wimbo huo katika studio za NoizMekah
production chini ya producer DX na amewashirikisha Jambo Squad.
Anasema hiyo itakuwa ngoma yake ya kwanza rasmi baada ya zile alizokuwa
katika maisha ya shule. Amesema itatoka baada tu ya mwezi wa ramadhani
kumalizika.
“Nina ngoma yangu ambayo natarajia kuitoa baada ya maisha skonga
kwasababu nilikuwa natoa nyimbo kwaajili ya wanafunzi, hazikuwa official
songs zangu, zilikuwa kama zawadi kwa wanafunzi,” ameiambia Hisia
“So now nakuja na ‘Serebuka’ nimefanya NoizeMekah Production chini ya
producer DX ni ngoma ambayo naamini itaniweka sehemu fulani katika
muziki. Natarajia hii ngoma itatoka baada ya mwezi wa ramadhani
kumalizika,naomba support wadau wangu.”
Post a Comment