Kanye
West ana mtu wa kumtetea kwa kitendo alichokifanya juzi kwenye uwanja
wa ndege wa LAX nchini Marekani. Rapper mwenye asili ya mkoani Singida,
Cyril aka Kamikaze, amemuunga mkono Yeezy aliyeamua kumfundisha adabu
mmoja wa mapaparazzi waliokuwa wamejaa kwenye uwanja huo wa ndege
kumpiga picha.
“Tunatokea mtaani ,tunajua jinsi yakua wahuni vile vile..majina u
fame usikudanganye …jichanganye uoneshwe michezo.. #ganstarganstar
#kanyewest katisha pu*bav zao maswala ya kuingiliana private life sio
issue..#badomimi #kudundamtu, “ameandika Cyril kwenye Instagram.
Hata hivyo, Kanye West sasa hivi anakabiliwa na kosa la jaribio la
unyang’anyi baada ya kujaribu kumnyakua paparazzi huyo aitwaye Danio
camera yake alipokuwa akiwasili kwenye uwanja huo wa ndege siku ya
Ijumaa.

إرسال تعليق