MBUNGE
wa Ubungo John Mnyika amewashauri vijana kutoa maoni bora yatakayowapa
fursa kushiriki kwenye uongozi wa taifa pindi wanapotoa maoni katika
mabaraza ya Katiba.
Mbunge
huyo kijana alisema hayo Dar es Salaam jana alipozungumza mkutano wa
baraza la vijana waliokuwa wakijadili rasimu ya Katiba mpya.
Alisema
licha ua uzuri wake bado rasimu hiyo ya awali ina upungufu hususan
kwenye maeneo yanayomzungumzia kijana huku akitoa mfano umri wa kuwania
uongozi wa juu wa kitaifa kutakiwa kuwa na zaidi ya miaka 40.
“Rasimu
ya Katiba ina mianya mingi ya ubaguzi kwa vijana mathalani kubadili
sifa ya umri wa mtu kuwa mbunge kutoka miaka 21 hadi 25 hii si sawa
sababu ukubwa wa umri sio wingi wa maarifa.
“Kwa
mara ya kwanza haki za vijana zimeingizwa kwenye Katiba ijayo… Ibara ya
43 kwenye rasimu ya Katiba imezungumzia haki na wajibu wa vijana,
lakini vitu hivyo havijaanishwa kinagaubaga.
“…Masikitiko
yangu ni kwamba ibara hii haina maana yoyote, ipo kama pambo tu haki
zimechanganywa changanywa,” alisisitiza Mnyika.
Kwa
mujibu wa mbunge huyo ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA
mgombea uspika au urais kutakiwa kuwa na miaka isiyopungua 40 ni ubaguzi
kwa vijana
إرسال تعليق