Mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Shabani Mrutu kwa mujibu wa
vitambulisho vyake na mtumishi wa idara nyeti serikalini ameuwawa kwa
kupigwa risasi tatu kifuani na watu wanaosadikika kuwa majambazi na
kufariki papo hapo katika eneo la Magereji Tegeta kibaoni jijini Dar es
Salasam.
Tukio hilo lililovuta hisia za watu wengi limetoea majira ya mchana
ambapo Bw. Mrutu alikuwa na gari lake namba T. 508 Ady akielekea
magereji na kuvamia gafla na majambazi kwa kumiminiwa risasi muda mfupi
baada ya kushuka.
Wekisimulia tukio hilo baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wamemwelezea
marehemu kuwa alikutwa na mauti baada ya kujibizana na watu hao
waliofika na pikipiki huku wakiulizana masuala yaliyowafanya kana kwamba
wanafamiana na kisha kuchukua begi lake muda mfupi baada ya kummiminia
risasi tatu kifuani.
Aidha upande wa mafundi gereji ambao walitaka kuficha majina yao
walieleza kumzoea afisa huyo kwa kutengeneza magari yake eneo hilo
ambapo hufika na maofisa wenzake kama ilivyokuwa leo ambao walitangulia
kufika gereji na kutoweka baada ya tukio hilo huku mwenyekiti wa kamati
ya ulinzi wa magereji hayo Muntazi Khan akieleza wasiwasi wa tukio hilo
kuhusishwa na mgogoro wa magereji hayo na mwekezaji.
Kamanda wa polisi mkoa wa kipolisi Kinondoni jijini Dar es Salaam Bw.
Camilius Wambura aliyewahi kufika katika eneo la tukio kuungana na
makachero wa jeshi hilo pamoja na kuomba ushirikiano wa walioshuhudia
tukio hilo alikiri marehemu kuwa mtumishi wa serikali na kuahidi
kuchukua hatua za haraka na kubaini wahusika na kuwafikisha katika
vyombo vya sheria
إرسال تعليق