Jumamosi
ya July 27 kwenye Kilinge cha Msasani Club jijini Dar es Salaam,
tulipata fursa ya kuzungumza na muimbaji mahiri wa kike nchini, Grace
Matata.
Kwenye mazungumzo hayo, Grace ambaye ni mama wa mtoto wa kike mwenye
miezi 11 sasa, Ella amezungumza kuhusu maisha yalivyobadilika baada ya
kuwa mama, kazi anayofanya zaidi ya muziki, collabo na Lady Jaydee,
studio iliyomtoa kimuziki Mlab, wanamuziki anaopenda kufanya nao kazi na
muziki anaopenda kusikiliza.
Kuhusu maisha yalivyobadilika baada ya kuwa mama
Inafanya malengo yako yabadilike priority zako zinabadilika kabisa.
Miezi 10 na something iliyopita nilikuwa nawaza tofauti sana but dakika
ile unapata mtoto unatakiwa ujielewe sababu ni maisha umekabidhiwa, if
you mess up, you mess her up, kwahiyo it changes everything. Mwanzo
unaogopa, baadaye unajifunza, baadaye unagundua kwamba ni blessing, it’s
a blessing every day.
Anachofanya kwa sasa tofauti na muziki
Right now nafanya kazi na kampuni moja wanaforward mizigo lakini soon ntaanza kufanya kazi na shipping line
Kuhusu ukimya wake kwenye muziki
Nadhani nilipojifungua mpaka a few months mpaka mwezi wa tano
nilikuwa nipo kimya sana sababu nilikuwa nimebase zaidi kwenye mtoto
lakini recently kazi zinaendelea kama kawaida.
Kuhusu kama bado yupo MLAB
MLAB na mimi mkataba wetu umefika mahali umeisha lakini MLAB
walitengeneza ile brand ya Grace Matata wakanisaidia nilipokuwa najaribu
kutengeneza sound yangu kwahiyo walinisaidia kukua na wamenifisha hapa,
siwezi kusema siko MLAB tena na siwezi kufanya nao kazi tena, NO. But
unavyozidi kwenda mbele unagundua kwamba inabidi ufanye vitu vingine
tofauti tofauti, ufanye kazi na watu wengine tofauti. Kwahiyo this time
around nataka kufanya kazi na watu tofauti.
Kuhusu kufanya collabo na Lady Jaydee
Tunaiongela mara nyingi sema Jaydee mambo mengi sasa hivi yamembana,
ana tour, ana nini, hajatulia sana na mimi pia this time nimehama kazi,
nimetoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine kwahiyo mambo yakawa ni
mengi sana lakini every day hakuna siku tunayokutana hatuongelei hilo
suala.
Kuhusu wasanii anaotaka kufanya nao kazi
East Africa, Collo, nampenda kweli Collo kwa rappers. Kwa waimbaji
nampenda sana Juliana. Kwa Tanzania Karola na Jaydee ofcourse.
Kuhusu muziki anaosikiliza
Kuhusu muziki anaosikiliza
Kwa Tanzania nampenda Ali Kiba, hakuna kitu ambacho amewahi kuimba
sijakipenda. Akina Ommy Dimpoz nawasikiliza. Kwa hip hop akina Stereo,
One, akina Nikki. Kwa nje napenda sana wanawake wanaopiga live
instruments, wanaopiga kama gitaa au piano.
Sikiliza Interview yote hapa
Post a Comment