Vijana hawa wanaungwa mkono na jeshi na hata wamepewa mafunzo kukabiliana na Boko Haram |
Takriban watu
20 wameuawa nchini Nigeria baada ya makabiliano makali kati ya makundi
ya vijana waliojihami na wapiganaji wa kiisilamu.
Hii ni kwa mujibu wa jeshi na vijana wanaotoa ulinzi kwa wanavijiji.
Kulingana na
vijana hao wanaotoa ulinzi kwa niaba ya serikali, wapiganaji walivamia
kijiji cha Dawashe kaskazini mwa nchi siku ya Jumamosi , kukabiliana na
wapiganaji hao wa kiisilamu ambao nao walilipiza kisisasi kwa kutumia
silaha nzito huku wakiwaua raia.
Kikundi hicho cha ulinzi kiliibuka mwezi Mei na kuanza harakati zake wakati huo.
Kimeahidi kusaidia serikali kupambana na wapiganaji wa Boko Haram.
Zaidi ya watu 2,000 wameuawa tangu mgogoro huu kuanza mwaka 2009.
Kundi la Boko Haram linasema kuwa linapigana dhidi ya serikali kutaka kuwa na utawala wa kiisilamu kote Nigeria.
Jeshi
linatizama wapiganaji hao kama washirika wake na hivyo limewapa mafunzo
kulisaidia katika harakati dhidi ya wapiganaji hao wa kiisialamu.
Kiongozi wa
vijana hao Aliko Musa alisema kuwa watu 25 waliuawa mjini Dawashe katika
jimbo la Borno ambalo ndilo kitovu cha harakati za Boko Haram.
Naye msemaji wa jeshi Haruna Mohammed Sani alithibitisha kuwa watu 20 waliuawa.
Post a Comment