KOCHA Arsene Wenger amepewa ruhusa kuamua kuhusu usajili ya Pauni Milioni 40 wa Luis Suarez.
Mshambuliaji huyo wa Liverpool ni
kipaumbe cha kwanza katika usajili wa Arsenal majira haya ya joto na
timu hiyo ya London tayari imetoa ofa ya awali ya Pauni Milioni 30
iliyokataliwa.
BIN ZUBEIRY imeripoti
mapema wiki hii namna ambavyo Gunners wameanza tena mazungumzo na
mabosi wa Merseyside juu ya ofa mpya ya Pauni Milioni 35.
Lakini klabu hiyo ya Anfield imeweka wazi kwamba, mchezaji huyo hawezi kupatikana chini ya bei wanayoitaka.
Mkwanja mrefu: Arsene Wenger amepewa ruhusa kutumia Pauni Milioni 40 kwa ajili ya Luis Suarez
Ofa ya Pauni Milioni 40 litakuwa jaribio tosha la kumng'oa Suarez anayetaka kuondoka Anfield majira haya ya joto.
Wakala wa Suarez, Pere Guardiola, alikuwa na majadiliano na Liverpool ambayo imekubali kusikiliza ofa.
Ofa hiyo itakuwa uamuzi mzito kwa Gunners ambao wanataka kumnasa mchezaji huyo mmoja kati ya watatu inayowataka sana.
Sambamba na Suarez, Wenger pia anafikiria kuwasajili Gonzalo Higuain na Wayne Rooney.

Sokoni: Wakala wa Suarez amesema ikiwa Arsenal itatoa ofa, Liverpool watatakiwa kuwasikiliza

Amerudi kazini: Brendan Rodgers na Liverpool wamerejea kwenye mazoezi ya kujiandaa na msimu
Kocha wa Liverpool, Brendan Rodgers anaamini Suarez ana deni ka wachezaji wenzake - na mashabiki wa klabu - la kubaki Anfield.
"Si kuhusu mimi au klabu, nafikiri mashabiki na wachezaji wenzake kwa kile wanachompa,"alisema.
"Wamekuwa naye kwa shida na raha, na kwa vipindi vyote alivyopitia kwa misimu zaidi iliyopita. Ikiwa kuna yeyote anayedai, ni wao ni wachezaji wenzake, ambao walipambana upande wake, hakika si mimi,".

Anateka hisia: Suarez amesema anapagawa na mpango wa kusajiliwa na wapinzani wa Liverpool katika Ligi Kuu England, Arsenal

Arsene Wenger akiwa kwenye ziara ya timu kujiandaa na msimu

Shakani: Usajili wa Higuain unaweza kukwama, na Wenger amehamishia mawindo yake sehemu nyingine
Wakati huo huo, beki wa Gunners, Bacary Sagna amesema hataondoka Arsenal - na anataka kuthibitisha anastahili Mkataba mpya.
Sagna, mwenye umri wa miaka 30, yupo
katika miezi 12 ya mwisho ya Mkataba wake na ana ofa kutoka Paris Saint
Germain, Anzhi na klabu za Mashariki ya Kati.
Mfaransa huyo amegoma kusaini Mkataba wa
mwaka mmoja zaidi, akiamini anastahili Mkataba mrefu na anajiandaa
kuondoka kama mchezaji huyu mwishoni mwa msimu.
Lakini licha ya utata wa Mkataba wake,
Sagna amesema anataka kubaki Uwanja wa Emirates na kuthibitisha
anastahili Mkataba wa maana.
"NafuraI kuchezea Arsenal. Naipenda timu
yangu, najitolea kwa asilimia 100 kwa ajili ya timu na wakati wote
naifanyoa mazuri. Bado nipo hapa.

Hapa pa kubaki: Bacary Sagna amesema anataka kubaki Arsenal

إرسال تعليق