Ponda awatembelea Farid gerezani


mussa-uamsho
  • Kiza kinapozidi kuwa kinene, alfajiri inaingia
“Waislamu wanatambua msimamo wenu wakupigania haki, pia wanaamini kukamatwakwenu ni ukweli wa methali isemayo ‘kizakinapozidi kuwa kinene, ndivyo kupambazukakunavyo karibia.”
VIONGOZI wa Jumuiyaya UAMSHO Zanzibar,wamesema kwambapamoja na kuzuiwakwao Gerezani, hawanashaka kuwa ipo siku hakiitasimama na hatimayekupatikana Taifa Uhurula Zanzibari.
Kauli hiyo wameitoambele ya Katibu wa Jumuiya na Taasisi zaKiislamu nchini, SheikhPonda Issa Ponda, mudamfupi baada ya kukutanana viongozi hao Ijumaaya wiki iliyopita katikaGereza la Kiinuamiguu,lililopo Mtaa wa KilimaniZanzibar.Sheikh Ponda, alifikagerezani hapo akiwa katikamuendelezo wa ziara zakeanazofanya nchini nakuongea na Waislamu, baada ya kumalizika kwakesi yake na kuhukumiwakifungo cha mwaka mmojanje.Akiongea na Mwandishiwa habari hizi katika ofisiza Baraza Kuu la Jumuiyana Taasisi za Kiislamu(T), Kinondoni, Jijini Dares Salaam, mapema wikihii alisema alifanikiwakuonana na viongozi waUAMSHO na kuongea naokwa muda wa dakika 45.
Alisema, Masheikhhao waliopo gerezanikwa muda wa miezi tisasasa, wapo imara kiimaniambao walitumia fursahiyo kumpa salamu kwaWazanzibari huku nayeakiwapa salamu kutokakwa Waislamu wa Bara.“Hawana hofu pamojana kushikiliwa na Dola kwamuda wote huo, kwaniwanachoamini wao kuwawapo katika haki, na uimarawao unakuja kutokanana kuijua vizuri historiaya kupigania haki kuwahata Mitume wa MwenyeziMungu, walipotangazahaki, walipata misukosukona kupigwa vita nawatawala.”
Alisema Shkh. Ponda, akielezeahali za Viongozi hao waUAMSHO.Ponda, alisema kuwaMasheikh hao, MselemAli, Azan Khalid, Musa Juma pamoja nae AmirFarid Had, kwa kwaujumla akiyatafakarimaongezi yao anaona
Na Bakari Mwakangwale ni wazi kuwa msimamowao ni kutorudi nyumakatika kupigania haki nazaidi alidai walimuambiahawana shaka kuwa iposiku haki itasimama na batili itaondoka Visiwanihumo.Alisema, Masheikh hao,walimtaka awafikishieujumbe Wazanzibar katikamikutano yake kuwawasiache kuzungumziahaki zao za msingiwanazodai kwani kwakufanya hivyo ndiyokuitendea haki Zanzibar.
“Katika fursa hiimliyoipata ya kuwahutubiaWazanzibar na hatimaeWatanganyika, waambienimsimamo wetu bado ni uleule wa kutetea Taifa Uhurula Zanzibari na bila shakapia huo utakuwa ni Uhurukwa Watanganyika pia”,alisema Sheikh Ponda,akimnukuu Amir FaridHad.
Sheikh Ponda alisemaviongozi hao walimuagizakutumia vema fursa yamikutano yake Visiwanihumo na hatimae Barakwa kuinua hamasa zaWaislamu huku wakimtakakuwaelekeza kutumia vemamafunzo na misimamowaliyoitoa juu ya Taifahuru la Zanzibar.“Darsa zetu bila shakazimejenga imani na akida,vilevile zinatosha kuwasemina za kujitambua.
Lakini pia tulijenga hamasakubwa na utayari wakutetea haki hadharani.Kama Waislamuhawatakiwi kurudi nyumawasinyamaze hata kidogo”,alisema Sheikh Ponda,akidai kuwa huo ni ujumbekutoka kwa Sheikh MselemAli.Awali Sheikh Ponda,kwa upande wake aliwapaviongozi hao salamu nahisia za Waislamu wa Barakufuatia ziara zake katikamikoa kadhaa ya TanzaniaBara zilizoandaliwa na Jumuiya na Taasisi zaKiislamu mara baada yakutoka Gerezani.
“Waislamu wa Barawanatambua msimamowenu wa kupigania haki,pia wanaamini kukamatwakwenu ni ukweli wa methaliisemayo ‘kiza kinapozidikuwa kinene ndivyokupambazuka kunavyokaribia’ hivyo wako pamojananyi.” Alisema SheikhPonda, akirejea kauli yakembele ya viongozi waUAMSHO Gerezani.Katika ziara yake hiyoVisiwani humo, SheikhPonda, pia alipatafursa ya kuwahutubiamaelfu ya Wazanzibarkatika mihadhara sitailiyoandaliwa na Jumuiyaya UAMSHO katikamaeneo mbalimbali yaUnguja.
Akiwahutubia maelfu yawaumini walio hudhuriakatika muhadharauliofanyika Mkoa wa MjiniMaghribi Masjid SahabaDaraja Bovu, Sheikh Ponda,aliwataka Waislamu waZanzibar kuchukua hadhariya njama zinazopikwakuvunja udugu wao kwalengo la kuwagawa.Kwa mujibu wa SheikhPonda, alisema maelfu yaWaislamu waliokutanakatika Msikiti wa harakatimaarufu kwa jina laMsikiti wa Mbuyuni,walisema wanatafakarihatma ya viongozi waowanaoshikiliwa na Dolakwa zaidi ya miezi tisasasa.
“Msimamo kama huoulitolewa tena katikamkusanyiko mkubwauliofanyika siku iliyofuata(Ijumaa iliyopita) maratu baada swala ya Ijumaakatika Msikiti wa kwaMpendae kwa Kificho.
Kuonesha hisia zenukama hivi bila shakamnajenga nguvu kubwaya pamoja na wakatiutakapofika watawatoatu viongozi wenu”.Alisema Sheikh Ponda,akiwahutubia waumini waNungwi.Aidha Shkh Ponda,aliwataka waumini waNungwi kujiimarishakwa miradi ya maendeleokwa kutumia vizurihazina kubwa ya ardhiwaliyonayo ambayoimekuwa ikivamiwa kwakasi kubwa na wawekezajiwa mahoteli ya kitalii,ambao kwa asilimia tisiniwanaharibu utamaduni waMzanzibar.
Sheikh Ponda, alisema Jumuiya ya UAMSHO,inatarajia kufanyamuhadhara mkubwa sikuya Ijumaa (leo) katikaMsikiti wa Mbuyuni,lengo likiwa ni kufanyamajumuisho ya mihadharailiyofanyika akiwa hukowiki iliyopita.

chanzo:annur

Post a Comment

أحدث أقدم