
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akijibu maswali toka kwa wanahabari wakati wa
mkutano wa pamoja na waandishi wa habari mara baada ya mkutano wa siku
moja wa Kamati ya Troika ya Siasa na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo
Kusini mwa Afrika (SADC Organ Troika on Politics, Defence and Security
Cooperation) katika jumba la wageni wa Rais la Sefako Makgatho jijini
Pretoria, Afrika Kusini, Jumamosi usiku. Kutoka kulia ni Rais wa Afrika
Kusini Mhe Jacob Zuma, Rais wa Msumbiji ambaye pia ni mwenyekiti wa SADC
Mhe Armando Guebuza, Katibu Mtendajji wa SADC Dkt Tomaz Augusto Salomão
na Waziri wa Mambo ya Nje wa Namibia Netumbo Nandi-Ndaitwah.

Ujumbe
wa Tanzania katika mkutano wa siku moja wa Kamati ya Troika ya Siasa na
Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC Organ Troika on
Politics, Defence and Security Cooperation) katika jumba la wageni wa
Rais la Sefako Makgatho jijini Pretoria, Afrika Kusini, Jumamosi usiku.

Mwenyekiti
wa Kamati ya Troika ya Siasa na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini
mwa Afrika (SADC Organ Troika on Politics, Defence and Security
Cooperation), Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongozana na Rais Jacob Zuma
wa Afrika Kusini na Rais Armando Guebuza baada ya mkutano wa kamati ya
Troika katika jumba la wageni wa Rais la Sefako Makgatho jijini
Pretoria, Afrika Kusini, Jumamosi usiku.

Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na viongozi wa Jumuiya za Watanzania
waishio Afrika ya Kusini leo Julai 21, 2013 jijini Pretoria, Afrika ya
Kusini, muda mfupi kabla ya kurejea nyumbani baada ya kuhudhuria mkutano
wa siku moja wa Kamati ya Troika ya Siasa na Usalama ya Jumuiya ya
Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC Organ Troika on Politics, Defence and
Security Cooperation).

Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa
Jumuiya za Watanzania waishio Afrika ya Kusini leo Julai 21, 2013 jijini
Pretoria, Afrika ya Kusini, muda mfupi kabla ya kurejea nyumbani baada
ya kuhudhuria mkutano wa siku moja wa Kamati ya Troika ya Siasa na
Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC Organ Troika on
Politics, Defence and Security Cooperation). Kutoka kulia ni Mwenyeiti
wa Chama cha Wataalam Watanzania waishio Afrika Kusini, Dkt Hamza
Mokiwa, Mwenyekiti wa Tanzania Women in Gauteng (TWIGA), Mama
Scholastica Kimario, Rais Kikwete, Balozi wa Tanzania nchini Afrika ya
Kusini Mhe Radhia Msuya, Kaimu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania
waishio Afrika ya Kusini Bw. Deusdedit Rugaiganisa na Bw. David
Mataluma, mratibu wa Vijana katika Jumuiya ya Watanzania.


Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya kumbukumbu na balozi pamoja
na maofisa wa ubalozi muda mfupi kabla ya kuondoka kurejea nyumbani
baada ya kuhudhuria mkutano wa siku moja wa Kamati ya Troika ya Siasa na
Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC Organ Troika on
Politics, Defence and Security Cooperation).

Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiomndoka leo Julai 21, 2013 jijini Pretoria,
Afrika ya Kusini baada ya kuhudhuria mkutano wa siku moja wa Kamati ya
Troika ya Siasa na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika
(SADC Organ Troika on Politics, Defence and Security Cooperation).

Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Balozi wa Tanzania nchini Afrika
Kusini Mhe. Radhia Msuya leo Julai 21, 2013 jijini Pretoria, Afrika ya
Kusini, muda mfupi kabla ya kurejea nyumbani baada ya kuhudhuria mkutano
wa siku moja wa Kamati ya Troika ya Siasa na Usalama ya Jumuiya ya
Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC Organ Troika on Politics, Defence and
Security Cooperation).PICHA NA IKULU
Post a Comment