Rais Kikwete azindua mradi wa Umeme, Barabara, Kivuko na wilaya mpya ya Kyerwa Mkoani Kagera.


Kivuko cha zamani kilichokuwa kikitumiwa na wananchi wa Ngara kuvuka mto Rusumo

Kivuko cha zamani kilichokuwa kikitumiwa na wananchi wa Ngara kuvuka mto Rusumo.
Kivuko kipya cha MV Ruvuvu katika mto Rusumo kilichozinduliwa na Rais Kikwete Jumamosi Julai 27, 2013
Kivuko kipya cha MV Ruvuvu katika mto Rusumo kilichozinduliwa na Rais Kikwete jana.
Rais Kikwete akihutubia umati Ngara
Rais Kikwete akihutubia umati wa wananchi wa Ngara.
Rais Kikwete akikata utepe kuzindua rasmi ujenzi wa barabara ya Kagoma-Lusahunga katika wilayani Biharamulo
Rais Kikwete akikata utepe kuzindua rasmi ujenzi wa barabara ya Kagoma-Lusahunga katika wilayani Biharamulo.
Rais Kikwete akiongea na wananchi katika sherehe ya kuzindua mradi wa umeme vijijini katika kijiji cha Nyaishozi, Wilaya ya Karagwe (2)
Rais Kikwete akiongea na wananchi katika sherehe ya kuzindua mradi wa umeme vijijini katika kijiji cha Nyaishozi, Wilaya ya Karagwe.
Rais Kikwete akisimikwa kuwa chifu wa Wahaya na kukakabidhiwa mgolole na silaha za jadi za Wahaya katika sherehe ya kuzindua wilaya mpya ya Kyerwa (1)
Rais Kikwete akisimikwa kuwa chifu wa Wahaya na kukakabidhiwa mgolole na silaha za jadi za Wahaya katika sherehe ya kuzindua wilaya mpya ya Kyerwa.
Rais Kikwete akisimikwa kuwa chifu wa Wahaya na kukakabidhiwa mgolole na silaha za jadi za Wahaya katika sherehe ya kuzindua wilaya mpya ya Kyerwa (2)
Rais Kikwete akisimikwa kuwa chifu wa Wahaya na kukakabidhiwa mgolole na silaha za jadi za Wahaya katika sherehe ya kuzindua wilaya mpya ya Kyerwa.
Rais Kikwete akipiga picha ya kumbukumbu na wananchi wa Ngara baada ya kuzindua kivuko cha MV Ruvuvu katika mto Rusumo Jumamosi Julai 27, 2013
Rais Kikwete akipiga picha ya kumbukumbu na wananchi wa Ngara baada ya kuzindua kivuko cha MV Ruvuvu katika mto Rusumo jana.
Rais Kikwete akishiriki kupiga ngoma na kikundi cha utamaduni cha Ngara wakati wa uzinduzi wa kivuko cha MV Ruvuvu katika mto Rusumo wilayani Ngara
Rais Kikwete akishiriki kupiga ngoma na kikundi cha utamaduni cha Ngara wakati wa uzinduzi wa kivuko cha MV Ruvuvu katika mto Rusumo wilayani Ngara.(Picha na IKULU).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Ijumaa, Julai 26, 2013, ameweka jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa Barabara ya Kagoma-Lusahunga katika Mkoa wa Kagera.
Rais Kikwete ameweka jiwe hilo la msingi nje kidogo ya mji wa Biharamulo ambako barabara hiyo inapitia ikiwa ni shehemu ya ziara yake ya siku sita katika Mkoa wa Kagera ambako anakagua shughuli za maendeleo.
Barabara hiyo yenye urefu wa kilomita 154 inagharimu kiasi cha sh.bilioni 196.6 ikiwa ni pamoja na fedha za ujenzi wenyewe ambazo ni sh.bilioni 191.6, fedha za kumlipa mshauri sh.bilioni 3.5 na fedha za kulipia fidia kwa ajili ya watu waliopoteza mali zao kupisha ujenzi wa barabara sh.bilioni 1.5.
Fedha zote za kugharimia ujenzi wa barabara hiyo zimetolewa asilimia 100 na ujenzi wenyewe umekamilika kwa asiliamia 96 na zimebakia kiasi cha mita 500 kwa ajili ya kumalizia barabara hiyo.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
26 Julai, 2013

Post a Comment

Previous Post Next Post