Kivuko cha zamani kilichokuwa kikitumiwa na wananchi wa Ngara kuvuka mto Rusumo.
Kivuko kipya cha MV Ruvuvu katika mto Rusumo kilichozinduliwa na Rais Kikwete jana.
Rais Kikwete akihutubia umati wa wananchi wa Ngara.
Rais Kikwete akikata utepe kuzindua rasmi ujenzi wa barabara ya Kagoma-Lusahunga katika wilayani Biharamulo.
Rais
Kikwete akiongea na wananchi katika sherehe ya kuzindua mradi wa umeme
vijijini katika kijiji cha Nyaishozi, Wilaya ya Karagwe.
Rais
Kikwete akisimikwa kuwa chifu wa Wahaya na kukakabidhiwa mgolole na
silaha za jadi za Wahaya katika sherehe ya kuzindua wilaya mpya ya
Kyerwa.
Rais
Kikwete akisimikwa kuwa chifu wa Wahaya na kukakabidhiwa mgolole na
silaha za jadi za Wahaya katika sherehe ya kuzindua wilaya mpya ya
Kyerwa.
Rais Kikwete akipiga picha ya kumbukumbu na wananchi wa Ngara baada ya kuzindua kivuko cha MV Ruvuvu katika mto Rusumo jana.
Rais
Kikwete akishiriki kupiga ngoma na kikundi cha utamaduni cha Ngara
wakati wa uzinduzi wa kivuko cha MV Ruvuvu katika mto Rusumo wilayani
Ngara.(Picha na IKULU).
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete,
Ijumaa, Julai 26, 2013, ameweka jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa
Barabara ya Kagoma-Lusahunga katika Mkoa wa Kagera.
Rais
Kikwete ameweka jiwe hilo la msingi nje kidogo ya mji wa Biharamulo
ambako barabara hiyo inapitia ikiwa ni shehemu ya ziara yake ya siku
sita katika Mkoa wa Kagera ambako anakagua shughuli za maendeleo.
Barabara
hiyo yenye urefu wa kilomita 154 inagharimu kiasi cha sh.bilioni 196.6
ikiwa ni pamoja na fedha za ujenzi wenyewe ambazo ni sh.bilioni 191.6,
fedha za kumlipa mshauri sh.bilioni 3.5 na fedha za kulipia fidia kwa
ajili ya watu waliopoteza mali zao kupisha ujenzi wa barabara sh.bilioni
1.5.
Fedha
zote za kugharimia ujenzi wa barabara hiyo zimetolewa asilimia 100 na
ujenzi wenyewe umekamilika kwa asiliamia 96 na zimebakia kiasi cha mita
500 kwa ajili ya kumalizia barabara hiyo.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
26 Julai, 2013
إرسال تعليق