KIUNGO wa Simba Mwinyi Kazimoto ameondoka nchini jana jioni kwenda Doha, Qatar kucheza soka la kulipwa, imefahamika.
Awali kulikuwa na taarifa kwamba nyota huyo aliondoka nchini jumapili iliyopita lakini vyanzo vya kuaminika viliiambia Hisia kwamba Kazimoto aliondoka jana (Alhamis) baada ya kutumiwa viza na wenyeji wake.
"Ilikuwa aondoke jumanne lakini viza yake ilikuwa haijatumwa hivyo ameondoka jana jioni,"kiliongeza chanzo hicho.
Kazimoto
ambaye pia ni mchezaji wa timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ anakwenda huko
kujiunga na timu moja inayoshiriki Ligi daraja la Kwanza.
Habari
za uhakika zilizopatikana jana zinaeleza kwamba nyota huyo anakwenda
huko baada ya klabu hiyo kuvutiwa na kiwango cha mchezaji huyo na hivyo
kufanya mchakato wa kumpeleka huko.
Imeelezwa
kwamba, kabla ya kusajiliwa rasmi kiungo huyo atafanyiwa majaribio na
iwapo atafuzu atasaini mkataba mnono ambapo utampatia kitita kinono.
Hata
hivyo, inadaiwa kwamba Kazimoto amekwenda huko bila ridhaa ya uongozi
wa klabu yake ya Simba wala timu ya Taifa ambayo alikuwa nayo kambini
kabla ya kutoweka ghafla baada ya mchezo wao na Uganda ‘The Cranes’
uliopigwa jumamosi iliyopita kwenye uwanja wa Taifa na Stars kuchapwa
bao 1-0.
Kazimoto
aliyejiunga na Simba mwaka juzi akitokea JKT Ruvu, inadaiwa kwamba
ameamua kwenda kujaribu bahati yake huko baada ya kuona hali si shwari
kwa upande wake katika klabu ya Simba.

إرسال تعليق