Mpendwa
Rihanna hivi hauamini ule usemi wa ‘malipo ni hapa hapa duniani’??
Inavyoonekana mashabiki wa ‘bad girl’ Rihanna aka Riri wameanza
kuchoshwa na tabia yake ya ‘uswahili’ wa kuchelewa kwenye maonesho yake,
na safari hii walimuandalia dawa yake kwa kuamua kummwagia chips
jukwaani baada ya kuchelewa kufika katika onesho lake la Diamonds huko
Manchester, Uingereza Jumanne (July 16) wiki hii.
Japo akili ya mwimbaji huyo wa Diamonds haikujiongeza haraka kuutumia
ule mwamvuli wake maarufu ‘Umbrella’ kujikinga na chips hizo kutoka kwa
mashabiki hao ambao pamoja na hasira lakini bado walimngojea kwa hamu.
Rihanna (25) alichelewa kwa saa moja tu, lakini hii si mara ya kwanza
kuchelewa katika matamasha yake na kuwafanya mashabiki waliofika kwa
wingi kumwona wapandwe na gadhabu. Mwezi (march) mwaka huu alichelewa
masaa 2 katika onesho lake la Montreal, Canada na (July 6) akiwa amelewa
chakali alichelewa tena masaa mawili katika show yake ya Poland.
Mrembo huyo wa Barbados baada ya kupokea zawadi hiyo (chips) kutoka
kwa mashabiki wenye gadhabu akiwa jukwaani alijibu mashambulizi hayo kwa
maneno makali “There’s a good crazy and there’s a bad crazy. When
you throw s*** up here, that’s an epic fail. I wanna get your gifts but
I don’t want you to knock my people out”.
Tazama video ya Rihanna akiongea na mashabiki baada ya tukio hilo
SOURCE:BBC

Post a Comment