Msanii
mwenye mistari iliyosimama katika hip hop, Stamina a.k.a.
‘Shorwebwenzi’wiki ijayo anatarajia kuachia ngoma mpya iitwayo ‘Mwambie
na Mwenzio.
Stamina amesema kuwa kazi hiyo ameirekodiwa Mwanza kwenye
studio za One Luv FX, chini ya mpishi Tiddy Hotterna kumshirikisha mkali
mwingine wa michano, Darasa.
Stamina amesema wazo zima la chorus ya ngoma hiyo limetoka kwa
Darassa na pamoja na mwanadada Wada ambaye ni mgeni katika ulimwengu wa
muziki nchini.
“Jina la ngoma mwambie na mwenzio linawakilisha mistari mikali ambayo
kila mmoja akiisikia atatamani kumwambia na mwenzie ujumbe ambao
atakuwa ameupata,” alisema Stamina.

Post a Comment