RIWAYA:ROHO MKONONI 21

Photo: RIWAYA:ROHO MKONONI
MTUNZI: George Iron

CALL: 0655727325

SEHEMU YA ISHIRINI NA MOJA

“Fonga…” sauti ya mshangao kutoka kwa Joyce!!.
“Beka kuzimu wanakuhitaji!! Ni hilo tu.” Alisema kwa hasira kiasi safari hii.
Beka akapagawa!! Hakika alikuwa amekamatika.
Wakati Beka akidhani kuwa mtu mwenye kumtia hofu ndani ya chumba kile ni Fonga peke yake, haikuwa hivyo!!
Vichwa vitatu ndani ya chumba kile vilikuwa vimekamilika haswa!
Alipojaribu kufurukuta, alijikuta akitua katika mikono ya mwanamama. 
Kilichomtokea hakukitegemea kutoka kwa mwanamke!!
Meno mawili yakadondoka chini.
Alipigwa kichwa kimojatuna yule mwanamama ambaye alikuwa kimya na hata alipomtoa meno hayo bado alikuwa kimya kama vile sio yeye aliyempiga na kichwa.
Beka akatua chini kama meno yake, sasa alikuwa amepiga magoti damu zikimtoka mdomoni.

PIGO lililoyaondoa meno mawili ya muheshimiwa Beka, ni mpigaji  pekee ambaye hakulishangaa lakini Fonga na mwenzake wakishirikiana na Joyce walilishangaa haswa. 
Pigo makini kutoka kwa mwanamke makini.
Fonga aligutuka na kutambua kuwa kilichowaleta ndani ya chumba kilikuwa hakijakamilika, alichukua kitambaa na kumfuta Beka damu kisha akaamuamuru kusimama. Beka alijaribu lakini ni kama lile pigo zito  lilimpa kizunguzungu sana. Akataka kuanguka mara akadakwa na yule mbaya wake aliyeyaondoa meno yake mawili.
“Beka yaani hivi tu unataka kuanguka bosi.” Kwa mara ya kwanza yule mwanamke alizungumza. Beka akamgeukia, wakatazamana!! Beka akataka kusema neno lakini kinywa kikawa kizito!! Hakuweza kusema lolote lakini ni kama alikuwa akimtambua yule mwanamke!!

*****

MALLE aliona kwa mbali ujio wa watu watatu majira ya usiku katika hoteli ile ya Rombo Green View, alitikisa kichwa chake na kujisikitikia kuwa kazi ya kumlinda mwanadamu ni ngumu sana, hasa hasa mwanadamu muovu mwenye maadui wengi wanaomzunguka.
Lakini hakuwa na jinsi maana bila kumtumikia Beka angekosa kula yake!!
Sasa alipowaona wale watu, kwa nidhamu ya kazi yake haramu hakutakiwa kuwaamini hata kidogo. Japo kwa mtazamo walionekana kama wapangaji wa kawaida katika hoteli.
Lakini wapangaji gani wanaongozana watatu kwa pamoja, wawili wanaume na mmoja mwanamke? Hili swali lilimvuta na kumfanya awape wenzake taarifa.
Wakajisogeza mapokezi baada ya wageni wale watatu kutoweka.
Wakiwa wanafahamika kama walinzi wa muheshimiwa, walipewa ushirikiano wahali ya juu sana.
“Ni akina nani watu wale?” aliuliza Malle.
“Ni polisi, wapo hapa katika kupeleleza tukio la mauaji yaliyotokea hapa jioni”alijibu kwa staha muhudumu wa kike.
Malle hakuridhika kabisa na maelezo yale, kwani ni muda mfupi uliopita polisi wengine walikuwa eneo lile. Halafu polisi gani hawa wanaongozana wote watatu kwa pamoja?  Si kawaida ya  polisi hata  kidogo kuongozana mithiri  ya kumbikumbi wakiwa katika upelelezi.
Hapana!! Alikata Malle katika kichwa chake, kisha akatoweka bila kusema neno. Akawaendea wenzake ambao walikuwa wakijiburudisha kwa bia kila mmoja akiwa na yake.
Alijaribu kuwaeleza juu ya hofu yake kuwa kuna watu wabaya wameingia eneo lile.
“Kwa hiyo unashauri nini Malle.”
“Wenye jukumu la kulinda chumba chake bora wawe jirani na eneo hilo kwa tahadhari tu lakini. Si mnamjua mzee vizuri….”alijieleza Malle.
“Tatizo lako Malle huwa muoga sana na unajifanya machale sana yaani.”alilalamika Rasi, mmoja kati ya vijana wa Beka. Ni  yeye alikuwa zamu ya kulinda chumba cha Beka akiwa katika tabia zake za  uzinzi.
“Halafu si unajua  bosi hapendi haya mambo ya kumsimamia mlango akiwa na Malaya wake?” Rasi aliendelea kujiwekea sababu kutokwenda kulinda chumba.
“Rasi eeh! Uamuzi ni wako lakini usije ukasema sikukueleza.” Alimaliza Malle kisha akaondoka kuelekea nje kabisa ya hoteli ile.
Rasi, akiwa amekasirika aliamua kutimiza wajibu. Akainywa bia iliyobakia katika chupa katika mfumo  wa tarumbeta.
“Oya Kenny, niangalizie hiyo simu  akipiga Suzi mwambie nimetoka kisogo lakini anisubiri nakuja”alihitimisha .
Kisha akatimua mbio kukiendea chumba cha Beka kilichokuwa ghorofani. Alipokifikia chumba akakiri kuwa Malle ni habari nyingine.
Machale yake yanaishi!!!
Alisikia vurugu ndani ya chumba, kulikuwa na majibizano ambayo hakuweza kuyasikia vizuri. Lakini palikuwa na lundo la watu katika chumba kile.
Rasi akaiweka vyema bunduki yake!! Akajibanza mahali ili aweze kuona nini kitatokea. Alingoja hadi mlango ulipofunguliwa.
Akamshuhudia bosi wake akisaidiwa kutembea, na ni kama alikuwa amejeruhiwa!! Rasi akabaki katika kigugumizi, afyatue risasi ama aendelee kuvuta subira.
Simu yake alikuwa ameiacha katika meza aliyokuwa ameketi na mwenzake hivyo asingeweza kuomba msaada kiurahisi.
Rasi alikuwa akijiuliza ni nani watu hawa, alihofia kuwakumba kwa kuhofia kuwa wanaweza kuwa askari hivyo kujikuta akimwingiza muheshimiwa katika matatizo mengine, kigugumizi hiki kilitoweka baada ya macho yake kutazamana na jambo la ajabu asilolitegemea.
Jambo ambalo likimkuta mtu mwingine yoyote yule lazima ashtuke na huenda akapiga kelele kabisa. Lakini Rasi hakupiga kelele.
Ni mwanadamu gani anaweza kutabasamu akikutana na mzimu wa mtu ambaye anamfahamu. Na mbaya zaidi ikiwa alishuhudia kwa macho yake kifo chake.
Rasi  alikuwa anatazama mzimu wa Fonga, kijana ambaye kifo chake kiliwapa ahueni na kufikia hatua ya kunywa pombe ili kujipongeza.
Sasa anamtazama akiwa hai tena kama kweli yupo hai.
Lakini alichoamini ni kwamba alikuwa akitazama mzimu ana kwa ana. Swali likamvamia kuwa ni kipi bora kupambana na mzimu wa Fonga na wenzake ama kuruhusu uoga na kisha bosi wake aendelee kusoteshwa na watu wale!! Kwa wakati huo hakuwa na wazo tena kuwa wale ni polisi. Alichoamini ni watekaji kama watekaji wengine.
Rasi akaruka hatua kubwa nne bila kuruhusu vishindo.
“Mikono juu wote. Simama hapo hapo bila kufanya vurugu zozote zile, la si hivyo napasua vichwa vyenu!!” sauti tulivu ya Rasi iliamrisha. Bunduki yake ndogo ikiwa inatazama visogo kadhaa.
Nguvu zikarejea katika mwili wake.
“That’s my boy Rasi.” Alijitutumua Beka, akazungumza huku akiruhusu damu zilizochanganyikana na udenda zimwagike chini.
Fonga alihisi miguu ikimlegea, Joyce akatokwa na yowe dogo la hofu na mshtuko. Mark hakujua nini cha kufanya. Mbaya zaidi hakujua maadui walikuwa wangapi na wamejipanga vipi.
Mark akajuta kumsaidia Fonga katika oparesheni hiyo
Mambo yalikuwa yamewageukia!!!
Mdomo wa bunduki ulikuwa tayari kutema risasi!!
Fonga kwa jicho la kuibiaibia akakutana na bunduki ambayo iliua mtu jioni ile. Pia akakutana na macho yale yale yaliyomtazama kabla hayajafyatua risasi. 
Fonga akakiri kuwa ngoma ilikuwa imemshinda!!!

****

UTOTONI lilionekana kuwa jambo la kawaida sana alipojichanganya na kucheza mpira wa miguu na wavulana, hakupendelea na wala hakuwahi kucheza michezo ya mdako ama baba na mama. Hili nalo halikuchukuliwa uzito wowote.
Alipoanza shule, sketi pekee aliyokuwa akivaa ni ile ya shule. Nguo zake za kushindia zilikuwa suruali ama kaptula. Zote za kiume.
Akiwa darasa la tano wakaanza kumtania ‘jike-dume’. Mwanzoni aliwavumilia, hakusema neno walipomtania. Lakini walipozidi kumtania akawabadilikia, alimkamata mvulana mmoja na kumfanya mfano. Kipigo alichokitoa kilimshangaza kila aliyeona.
Hakuna aliyeamini kama yule aliyepokea kipigo kile alikuwa ni mvulana mkubwa tu na aliyetoa kipigo ni msichana.
Ikabakia kuwa simulizi!! Utani ukakoma.
Alipomaliza darasa la saba, wazazi wake walifariki katika kile kilichoitwa imani za kishirikina. 
Husna akabakia kuwa mpweke!! Tena yatima.
Ukorofi wake ukamsababisha  akose  ndugu wa kuishi naye, na ile tabia yake ya kupenda kuwa mwanaume ikamsababisha akose mvuto.
Hii ikawa safari ya Husna kuingia mtaani akijichanganya na watoto wa kiume katika kupigania maisha kama Chokoraa. Maisha ambayo alilazimika kuyamudu. 
Asingeyamudu ni wapi angekimbilia?
Akiwa na miaka kumi na nane tu, alihukumiwa kwenda jela mwaka mmoja na nusu baada ya kumpiga dada mmoja ambaye alikuwa akifanya naye kazi ya ‘ubaamedi’. Kosa lilikuwa lile lile kumuita ‘jike-dume’. Kipigo alichompa yule dada kilipelekea mimba yake kutoka.
Mahakama ikamuuliza Husna kama angeweza kuilipa mimba ya miezi mitano, Husna akashindwa na kuambulia hukumu hiyo ya miezi kumi na nane
Ni katika maisha ya ufungwa wake ndipo alipobatizwa jina la ngumi jiwe. Hii  ilitokana na vichapo alivyokuwa akivitoa wakati akitumikia adhabu hiyo. Hakuna aliyemtetemesha binti huyo wa ajabu ambaye alikuwa akifanya mazoezi ya ndondi wakati akiwa uraiani. Wanyampara wakamuita ‘ngumi jiwe’. Jina hili likamkaa.
Aliporejea uraiani, wale wasichana aliokutana nao jela wakalileta jina lile mtaani. Husna Ngumi jiwe!!
Baada ya kutoka jela alihaha kujiweka katika mstari, lakini kwa mara nyingine tena akaangukia katika ubaamedi. Ni huku ambapo alikutana na Mark B, kijana wa miaka ishirini na tano. 
Mtukutu anayejua nini maana ya utukutu, huyu akamuingiza Husna katika harakati za kusaka pesa kwa njia zisizokuwa halali. 
Kilichomsababisha Mark avutiwe na Husna ni ujasiri wa Husna na pia kamahilo halitoshi, Husna alikuwa na machale, kitu ambacho watu wachache walikuwa nacho. Kabla ya kumchukua alikuwa amempa mitihan ni mingi bila kujua kama alikuwa akmipewa mitihani.
Mark akatambua kuwa Husna ni nguzo imara sana.
Katika tukio la kwanza Husna hakushiriki ipasavyo, lakini hili la pili Husna ngumi jiwe amesambaratisha meno mawili ya mzee Beka ambaye aliwahi kumsumbua sana enzi hizo akiwa baamedi.
Sasa sio baamedi tena!!

Wakati Fonga akihaha na kukaribia kujikojolea, Joyce akiwa anatetereka na  asijue ni kitu gani kinaendelea duniani, Mark ambaye  naye alikuwa amenyanyua mikono juu alikuwanusu ana matumaini  na nusu akiwa anaona dalili ya kufikia  mwisho wa kufadhaisha.
Lakini akiwa bado na utata akilini mwake, likatokea jambo ambalo alikuwa hatarajii.

Husna ambaye aliwaruhusu wenzake watangulie nje ya chumba wakiwa na Beka, yeye aliendelea kupekua chumba kile bila kujuani kitu gani alikuwa akikagua.
Lakini  jibu alilipata baada ya kumaliza kupekua kitukisichojulikana. Alipotoka nje akakumbana na kijana mgeni akiwa ameielekeza bastola yake katika visogo vya Mark, Joyce na Fonga.
Upesi alikivua kiatu chake kilichokuwa na kisigino kirefu. Akaanza kunyata, wakati akinyata mzee Beka naye alikuwa  anageuka upande  aliokuwepo. 
Hapa ukaibuka mchezo wa ujanja kuwahi. Husna hakurejea nyuma, alijionya kwa kauli ya. Adui mfuate!!
Beka alikutanisha macho yake na kiwiliwili cha Monica. Kwa jinsi ambavyo alikuwa ametokwa damu hata hakuweza kuonekana kama alikuwa amekodoa macho, Beka  alijaribu kunyanyua mkono wake ili aweze kumwonyesha Rasi hatari  iliyokuwa nyuma yake lakini mkono ule haukunyanyuka badala yake akakosa muhimili na kupinduka chini. Husna akaitumia fursa hiyo kucheza utaalamu wa ajabu ambao ungeweza kuondoka na roho yake.
Husna alitambua kuwa roho tatu zilikuwa mikononi mwake, na pia alikuwa na jukumu kubwa la kuikoa roho yake. 
Akakirusha kiatu pekee alichokuwa nacho  mkononi katika upande wa mbele wa Rasi mlinzi wa Beka.
Rasi naye akafanya makosa ya kijinga ya kuhadaika, akageuka ghafla kutazama ni wapi mlio huo ulipotokea.
Husna akaruka upesi na sasa alikuwa amemfikia Rasi, hakumsubiri ageuke, akajivuta nyuma kwa nguvu kisha akafyatuka na kichwa kikali, kikatua katika kisogo cha Rasi, akakohoa kidogo kisha akalegea taratibu na kusalimiana na sakafu!!
Kisha konde moja zito likatua katika uso  wa Beka ambao ulikuwa umeanza kuchanua kwa tabasamu hafifu.  Beka akapoteza fahamu rasmi!!
Fonga, Mark na Joyce wakabaki kuduwaa wakimtazama Husna asiyekuwa na hofu wala mchecheto wa aina yoyote.
“Twende  zetu ama!” alisema Husna, na hapo kila mmoja akili ikasogeleana upya.  Wakatambua kuwa wapo kazini.
“Vipi huyu sasa?” Mark alimuuliza Husna.
“Huu mzoga tu achana nao.” Alijibu huku akiukanyaga mwili wa Rasi na upesi wakatoweka eneo lile wakijiamini kabisa kwani tayari walijitambulisha kama askari mapokezi pale.
Huku wakiuburuta mwili uliuopoteza fahamu wa muheshimiwa Beka, walifika mapokezi. Afande feki Mark alitoa shukrani kisha wakaanza kutoka nje na mzoga wao.
Baada  ya kumtoka Rasi kiwepesi, wakafikia himaya ya nje ambayo ilikuwa chini ya vijana wawili tu ambao walijifananisha na makomandoo wa kivita.
Kenny  (Rambo) na Malle!!
Vijana wasiokubali kushindwa kirahisi, vijana wasioogopa kuua dakika yoyote ile. Silaha kali katika himaya yao na pia wakiona fahari kuwa kama walivyo.
Kundi dogo la akina Fonga ambalo halikuwa limejipanga ki-silaha, likajikuta  limecheza makosa mawili ambayo yaliubadili usiku huu kuwa usiku wa machozi na damu!!

Huku nyuma Rasi alirejewa na fahamu, huku nje Malle na Rambo walikuwa moto wa kuotea mbali katika kitu kinachoitwa ulinzi wa nje.  Rambo mtaalamu katika mashambulizi ya kutumia silaha. Huku upande mwingine Malle akiwa bingwa wa machale.
Na kwa sababu alishachezwa machale mapema juu ya watu wale waliojitambulisha kama askari. Aliwangoja wakitoka aweze kuthibitisha utambulisho wao.

***MPAMBANO ndo kwanza umeanza…kumbuka Betty hajulikani alipo na kutekwa kwake ndo chanzo cha haya yote….
**ROHO Kadhaa zipo katika hatihati ya kupotea!!!  

NINI KITAENDELEA….
ITAENDELEAKESHO
#Bofya LIKE, tupia COMMENT na ikibidi SHARE

RIWAYA:ROHO MKONONI

ITAENDELEA
#Bofya LIKE, tupia COMMENT na ikibidi SHARE

Post a Comment

أحدث أقدم