Kampuni
ya Samsung imeweka record nyingine baada ya kumpita mpinzani wake Apple
kwa kutajwa kuwa kampuni ya simu za mikononi ‘smart phone’
inayotengeneza faida kubwa zaidi duniani kwa sasa.
Kwa mujibu wa wachambuzi wa sekta hiyo Kampuni ya Apple imejikuta
ikiporomoka sokoni kwa 14% katika kipindi cha miaka mitatu kutokana
na kutofanya vizuri katika toleo lake la iPhone 5 pomoja na ushindani
mkubwa kutoka kwa wapinzani hasa Samsung.
Samsung kampuni ya Kikorea inakadiriwa kutengeneza faida inayofikia
£3.4billion kupitia simu zake za mkononi za Android katika kipindi cha
robo ya pili ya mwaka huu na kutengeneza asilimia 27.7 ya simu zote za
mkononi zilizouzwa sokoni mwaka huu.
Wachambuzi wameendelea kusema mauzo ya simu aina ya iphone
zinazotengenezwa na Apple yamekuwa chini ya kiwango kwa £3billion kwa
mujibu wa utafiti uliofanywa na Strategy Analytics.
Simu za iphone zimeendelea kupata upinzani mkubwa kutoka kwa Samsung
hasa baada ya kampuni hiyo ya kikorea kutambulisha Galaxy S4
iliyochangia Samsung kufanya vizuri zaidi sokoni kwa kipindi cha
karibuni.
Hata hivyo wataalam wanasema Apple inauwezo wa kuipita tena Samsung endapo watazindua toleo lijalo la iphone.
SOURCE: DAILY MAIL
إرسال تعليق