Baraka
za mwezi Mtukufu wa Ramadhan, zimeitembelea familia ya Baba Qayllah,
Shetta Bilal. Baada ya miaka mingi ya maelewano hafifu na baba yake
mzazi, leo baba na mwanae wameamua ‘kuLizika shoka’ (bury the hatchet)
na kuanza ukurasa mpya.
Kupitia Instagram, Shetta amepost picha (hiyo juu) akiwa na baba yake
mzazi Mzee Bilal ambaye ni Sheikh, pamoja na mdogo wake Awab na
kuandika: Wit my daddy n my young broda Awab….. #happyday baada ya miaka
mingi kuwa na tofauti na mzee tangu nina miaka 7 leo yameisha #bassawa
#Ramadankareem.”
Bongo5 imezungumza kwa simu na Shetta kutaka kupata maelezo zaidi ya kwanini alikuwa haelewani na baba yake.
“Basi tu tulikuwa tunakosana, nahisi situations zangu na maisha yangu
vilikuwa haviko sawa. Kazi yangu ninayofanya na nini kwasababu yeye ni
mtu wa dini sana, baba yangu ni Al Haj, Sheikh. Kwahiyo nahisi hilo
lilikuwa tatizo kwa upande wake..”
Shetta amesema kwa muda wote huo baba yake alikuwa hamfahamu mke wake
pamoja mwanae, Qayllah lakini sasa anafuraha kwakuwa wameyamaliza bab
yake amemuelewa.
Msikilize zaidi hapa:

إرسال تعليق