Katibu Mkuu
wa Chadema,Dk Willibrod Slaa amesema Tanzania haiwezi kuendelea kuwa na
amani kama wizi wa rasilimali za taifa utaendelea.
Dk Slaa
aliyasema hayo Dar es Salaam jana, wakati alipofungua mkutano wa Bodi ya
Kimataifa ya Shirikisho la Vyama vya Kidemokrasia kwa Vijana (IYDU)
ambao unafanyika kwa mara ya kwanza katika nchi za kusini mwa Jangwa la
Sahara.
“Amani
inakuwapo mahali penye haki” alisema Dk Slaa na kutolea mfano wa askari
ambao wamekuwa wakikamatwa na nyara za taifa wakati wao ni vyombo vya
dola, huku pia akisema migogoro ya ardhi inayokithiri inaweka rehani
amani ya taifa hili.
Haki
nyingine alizolalamilia Dk Slaa ni pamoja na kuminywa kwa demokrasia
ambapo ametolea mfano wa polisi kuzuia mikutano ya Chadema huku
akiwatuhumu kuwa wamekuwa mashabiki wa siasa badala ya kutimiza wajibu
wa kulinda amani kwenye mikutano hiyo.
Kuhusu msajili wa vyama vya siasa John Tendwa, Dk Slaa alisema Chadema walishamfuta kwenye orodha ya watu wanaowasiliana nao.
Akizungumzia
mpango wa chama hicho kuanzisha kikosi cha ulinzi, Katibu huyo alisema
hata kwenye majumba ya kawaida watu wanakuwa na walinzi wao iweje wao
kama chama wasifanye hivyo.
“Kuna walinzi wengi tu wanalinda majumba ya watu mjini, ni sheria gani inayotukataza sisi?” alihoji Dk Slaa.
Kwa upande
wa ajira alisema, hakuna nchi inayoweza kuwa na uchumi imara kama vijana
wake hawana ajira. Naye Mwenyekiti wa IYDU, Aris Kalafatis alisema
ujumbe wao mkubwa kwa vijana wa Tanzania ni kutaka mabadiliko hususan
katika masuala ya maendeleo,huduma za jamii na ukosefu wa ajira.
Akizungumzia
migogoro mingine inayotokea katika mataifa kama Misri na Tunisia,
Kalafatis alisema hawaungi mkono kudai haki kwa njia za machafuko,
wanachohitaji ni kuona migogoro inatatuliwa kwa njia za mazungumzo na
siyo kama hali ilivyo sasa
Post a Comment