Mnyika: Vijana piganieni umri Katiba mpya

MBUNGE wa Ubungo John Mnyika amewashauri vijana kutoa maoni bora yatakayowapa fursa kushiriki kwenye uongozi wa taifa pindi wanapotoa maoni katika mabaraza ya Katiba.
Mbunge huyo kijana alisema hayo Dar es Salaam jana alipozungumza mkutano wa baraza la vijana waliokuwa wakijadili rasimu ya Katiba mpya.
Alisema licha ua uzuri wake bado rasimu hiyo ya awali ina upungufu hususan kwenye maeneo yanayomzungumzia kijana huku akitoa mfano umri wa kuwania uongozi wa juu wa kitaifa kutakiwa kuwa na zaidi ya miaka 40.
“Rasimu ya Katiba ina mianya mingi ya ubaguzi kwa vijana mathalani kubadili sifa ya umri wa mtu kuwa mbunge kutoka miaka 21 hadi 25 hii si sawa sababu ukubwa wa umri sio wingi wa maarifa.
“Kwa mara ya kwanza haki za vijana zimeingizwa kwenye Katiba ijayo… Ibara ya 43 kwenye rasimu ya Katiba imezungumzia haki na wajibu wa vijana, lakini vitu hivyo havijaanishwa kinagaubaga.
“…Masikitiko yangu ni kwamba ibara hii haina maana yoyote, ipo kama pambo tu haki zimechanganywa changanywa,” alisisitiza Mnyika.
Kwa mujibu wa mbunge huyo ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA mgombea uspika au urais kutakiwa kuwa na miaka isiyopungua 40 ni ubaguzi kwa vijana

Post a Comment

Previous Post Next Post