Mkuu wa
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bi.
Joyce Mkinga (Kulia) akizungumza na wanahabari (hawapo pichani)
alipokutana nao kuzungumzia hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa Dira
ya Taifa ya Maendeleo 2025 na Utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa
Miaka Mitano (2011/12 -2015/16) jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bi.
Joyce Mkinga (Kulia) akionesha nakala ya Kijitabu cha Dira ya Taifa ya
Maendeleo (TDV 2025), alipokutana na wanahabari kuzungumzia hatua
iliyofikiwa katika utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 na
Utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2011/12 -2015/16)
jijini Dar es Salaam.
Na Georgina Misama-MAELEZO
Jumla
ya shilingi trilioni 44.5 za kitanzania zinatarajiwa kutumika katika
utekelezaji wa mpango wa maendeleo wa miaka mitano, ambapo Tanzania
imedhamiria kufikia hadhi ya nchi zenye kipato cha kati na kuondokana na
umaskini uliokithiri ifikapo mwaka 2025.
Hayo
yamesemwa Jijini Dar es Salaam na Mkuu wa kitengo cha mawasiliano,
Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango Joyce Mkinga alipokutana na waandishi wa
habari kuzungumzia utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo.
Joyce
alitaja malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo, ambapo alisema katika
miaka mitano ya kwanza vipaumbele vipo katika makundi ya Miundombinu
ambayo inahusisha nishati, usafirishaji, TEHAMA, maji safi na maji taka
na umwagiliaji, Kilimo ikijumuisha mazao ya chakula na biashara,Viwanda,
Rasilimali watu na uendeshaji wa huduma za utalii, Biashara na fedha ni
miongoni mwa vipaumbele vitano vya Taifa ambavyo serikali inatarajia
kutekeleza.
“Mkazo
mkubwa unatiliwa katika miradi ya maendeleo, tunaamini miradi
ikiendelea vizuri, umasini utapungua. Tume ya mipango ina wajibu wa
kufatilia miradi iliyowekewa kipaumbele na utekelezaji wake” alisema
Joyce Mkinga.
Aidha
Bi. Joyce alisema kuwa ili kufikia malengo jumla ya shilingi tirioni
8.9 zinahitajika kwa mwaka na kuongeza kuwa Serikali inakadiria kuwekeza
kiasi cha wastani wa takriban shilingi trilioni 2.9, kwa mwaka wakati
wastani wa shilingi trilioni 6.0 kwa mwaka zinatarajiwa kutokana na
uwekezaji binafsi au ubia.
Itakumbuwa
kuwa mpango wa matoke sasa ambao ulizundiliwa ambao ulizundiliwa na
Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mpango huu umelenga kuhakikisha utekekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 inafiiwa ifikapo mwaka 2025.
إرسال تعليق