January Makamba akizundua rasmi tuzo |
Naibu
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Ndugu January Makamba,
leo amezizindua rasmi tuzo za kwanza vijana walio chini ya miaka 30
(Under-30 Youth Awards) zinazotolewa na taasisi ya Youth For Africa
(YOA).
Picha Na:- bongo5.com
Mkurugenzi Mkuu wa YOA, Awadh Milasi
Uzinduzi wa tuzo hizo umefanyika kwenye kituo cha ubunifu wa masuala
ya Teknolojia ya Habari na Masiliano, ICT cha Kinu kilichopo jijini Dar
es Salaam na kuhudhuriwa na baadhi ya vijana waliotajwa kuwania tuzo
hizo, wadhamini na wadau wengine muhimu.
Fredrick Bundala, Bongo5 akikabidhi tshirt
Mmoja wa vijana wanaowania tuzo hizo, Gavin Gosbert mwenye koti
Licha ya kufanya uzinduzi huo, Ndugu Makamba pia ametoa vyeti kwa vijana waliotajwa kwenye tuzo hizo.
Akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kutoa vyeti hivyo,
Makamba ameipongeza taasisi ya YOA kwa kuanzisha tuzo hizo kwakuwa
zitawapa moyo vijana ili waendelea kujituma zaidi. Aidha amewashauri
waandaji kuzitanua zaidi tuzo hizo ili ziwatambue pia vijana waliopo
kwenye mikoa mingine nchini.
“Hili ni jambo jema tunaliunga mkono na tunadhani kwamba lisiishie
Dar es Salaam peke yake, wapo vijana wengi kwenye mikoa yote Tanzania
ambao wanatoa mchango mkubwa sana kwa maendeleo ya jamii yetu katika
Nyanja mbalimbali na wenyewe lazima watambulike, lazima tuwatuze na
kuwatia moyo,” alisema.
Akizungumzia kuhusiana na tatizo la ajira kwa vijana nchini, January
ametoa wito kwa vijana kujituma na kutokata tamaa na kuzingatia suala la
nidhamu.
“Wakati mwingine sio kile ulichosemea ung’ang’anie ufanye hicho
hicho tu, wapo vijana wengi ambao wamesomea kitu kimoja, wametafuta na
kuona fursa kwenye mambo mengi na wenyewe wamefanya.”
Akielezea kuhusu vigezo vilivyotumika kuyapata majina ya wanaowania
tuzo hizo naye Mkurugenzi Mkuu wa YOA, Awadh Milasi amesema majina hayo
yamepatikana kwa njia ya wazi na halali.
“Tumejaribu kutengeneza grounds of fairness. Tukizungumzia umri
unategemea hawa vijana ambao wapo shule ya sekondari, chuo au wamemaliza
chuo au ndio kwanza wameingia kazini. Lakini vile vile hatuangalii
rangi, dini, kabila kikubwa ni ule mchango waliofanya,”alisema.
January Makamba
January Makamba kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa YOA
MC
Michael Mbwambo, Popote Media
Nsia Swai, Onspot Magazine
Osse Sinare na Pedaiah Swank
Picha ya pamoja ya mgeni rasmi na wadhamini wa tuzo hizo
height=”533″ class=”aligncenter size-full wp-image-48505″ />
Picha ya pamoja ya vijana waliotajwa kwenye tuzo hizo
Picha ya pamoja ya vijana waliotajwa kwenye tuzo hizo
Tuzo hizo zinatarajiwa kutolewa August 17
Picha Na:- bongo5.com
Post a Comment