
Tanzania inapendekeza kufanyiwa,
marekebisho sheria ya kulinda amani, kuwezesha vikosi vya kulinda amani
kujikinga na mashambulizi.
Hii ni baada ya walinda amani saba wa Tanzania kuuawa na watu waliokuwa wamejihami eneo la Darfur mwishoni wa wiki.
Wanajeshi wengi walijeruhiwa baadhi wako mahututi.
Mauaji ya walinda amani 7 wa Tanzania nchini
Sudan imewashangaza wengi sana nchini humo kulingana na naibu waziri
mkuu kwani nchi hiyo ndio imeanza kushika kasi katika juhudi zake za
amani kimataifa. .
Maafisa hawakuwa na taarifa kamili kuhusu
uvamizi wa Jumamosi ambapo wanajeshiu wengine 17 walijeruhiwa vibaya
katika shambulizi baya zaidi kushuhudiwa dhidi ya vikosi vya kimataiofa
nchini Sudan.
Shambulizi hilo lililofanywa na kikundi kikubwa
cha watu waliokuwa wamejihami, ilihusisha mashambulizi makali ya mizinga
na iliyolenga wanajeshi hao umbali wa kilomita 25 Magharibi mwa mji wa
Khor Abeche.
Tanzania, ambayo pakubwa ni nchi salama na
thabiti katika Kanda ya Afrika Mashariki, imeendelea kujitolea sana
katika juhudi za amani duniani.
Mwaka jana ilikuwa nchi ya kwanza kujitolea
kupeleka vikosi vyake Mashariki mwa Congo, chini ya kile ambacho
kitakuwa kikosi cha walinda amani wa Umoja wa Mataifa wenye jukumu la
kupambana vilivyo na makundi ya waasi huko
إرسال تعليق