Umoja wa Mataifa kupeleka majeshi Goma.


GOMA
Umoja wa Mataifa umesema uko tayari kupeleka wanajeshi mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo kupambana na waasi, baada ya waandamanaji kuwatuhumu wanajeshi wa kulinda amani kutokuwa imara.
Msemaji wa Umoja wa Mataifa Martin Nesirky, amesema kuwa kikosi cha kulinda amani cha Kongo-MONUSCO, hakijawahi kushiriki katika vita.
Mapigano kwenye eneo la Goma yamesitishwa, lakini maandamano yamefanyika mjini humo, waandamanaji wakikituhumu kikosi cha Umoja wa Mataifa kutokuwapa wanajeshi wa serikali msaada wa kutosha.
Kikosi kipya cha brigedi kitaingia Goma kupambana na M23 na makundi mengine yenye silaha.

Post a Comment

Previous Post Next Post