
Umoja
wa Mataifa umesema uko tayari kupeleka wanajeshi mashariki mwa Jamhuri
ya Kidemokrasi ya Kongo kupambana na waasi, baada ya waandamanaji
kuwatuhumu wanajeshi wa kulinda amani kutokuwa imara.
Msemaji
wa Umoja wa Mataifa Martin Nesirky, amesema kuwa kikosi cha kulinda
amani cha Kongo-MONUSCO, hakijawahi kushiriki katika vita.
Mapigano
kwenye eneo la Goma yamesitishwa, lakini maandamano yamefanyika mjini
humo, waandamanaji wakikituhumu kikosi cha Umoja wa Mataifa kutokuwapa
wanajeshi wa serikali msaada wa kutosha.
Kikosi kipya cha brigedi kitaingia Goma kupambana na M23 na makundi mengine yenye silaha.
إرسال تعليق