
Fina Mango na Tundu Lissu katika picha ya pamoja katika studio za Magic FM.

Tundu Lissu Akizungumza katika Kipindi cha Makutano na Fina Mango

Fina Mango Akimsikiliza Tundu Lissu wakati akijibu moja ya maswali.

Muandaaji wa kipindi cha Makutano, Fina Mango akimshukuru Tundu Lissu kwa kufika studio
--
Mbunge wa Singida Mashariki, Mheshimiwa
Tundu Lissu amesema Muungano wa Tanzania umekufa kikatiba. Lissu
aliyasema hayo wakati alipoulizwa msimamo wake juu ya rasimu ya katiba
na muundo wa serikali katika kipindi cha Makutano kinachoendeshwa na
Fina Mango, Magic FM. Akijibu swali hilo alitolea mfano wa wakati wa
maadhimisho ya siku ya mapinduzi ya Zanzibar ambayo alisema anaekagua
gwaride na kupigiwa mizinga 21 anatakiwa kuwa rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania ambaye ndiye amiri jeshi mkuu lakini kwa sasa
katika maadhimisho hayo rais wa Zanzibar ndiye anayefanyiwa yote hayo
kutokana na katiba ya sasa ya Zanzibar kuitambua Zanzibar kama nchi.
Alisema "Katiba ya sasa ya Zanzibar
inasema rais wa Zanzibar ni mkuu wa nchi ya Zanzibar, ni kiongozi wa
serikali, ni kamanda mkuu wa vikosi vya idara maalum. Kimsingi sababu
kubwa ya Muungano ilikuwa ni masuala ya ulinzi na usalama na Zanzibar
imeyaondoa kwenye Muungano" na kumalizia kusema kuwa katiba ya sasa ya
Zanzibar ya leo ni waraka wa Uhuru.
Lissu alimalizia kwa kusema namna pekee
ya kubaki na Muungano ni kuwa na serikali tatu huku akiwakosoa
wanaosema mapendekezo ya tume ya katiba kuwa serikali tatu ni gharama
wanakosea kwani hakutakuwa na gharama kubwa kwa kusema kutakuwa na jumla
ya wabunge 314 tu tofauti na sasa ambapo kuna jumla ya wabunge 438 tu.
Hata hivyo alipoulizwa kama CHADEMA inaona kuna haja kuwepo Muungano
alisema ipo na kuongezea "Ndoa ya kulazimishana hapana, kama upande
mmoja unataka out is out".
Lissu alimalizia kwa kusema wananchi wa kawaida wa Zanzibar hawautaki Muungano kwani hawaoni faida yoyote.
Katika Mahojiano hayo ya muda wa saa zima, Tundu Lissu aliongelea mambo mbalimbali ikiwemo suala la kodi ya kadi simu.
Post a Comment