WAZIRI MKUU PINDA KUSHTAKIWA MAHAKAMA KUU


Dar es Salaam, Tanzania. 
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC)  kimesema kwamba kinajiandaa kumshtaki Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kutokana na kauli yake alioitoa hivi karibuni kwamba ‘wapigwe tu’.

Kituo hicho kimesema kwamba Pinda anapaswa kushtakiwa kwa kuwa amevunja kifungu cha katiba ya Usawa mbele ya sheria  ibara 13 (1).

Hivi karibuni Waziri Mkuu, Pinda akiwa bungeni alisema serikali imechoshwa na vurugu zinazotokea mara kwa mara na kwamba hakuna namna nyingine ya kuwadhibiti raia wanaowadhuru vyombo vya dola zaidi ya kuwapiga.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Maboresho na Utetezi wa kituo hicho Harold Sungusia wakati akitoa ripoti ya utafiti ya miezi sita kuhusu mambo mbalimbali yanayolenga haki za binadamu.

Sngusia amesema kituo hicho kiko katika hatua za mwisho za kupeleka shauri hilo katika Mahakama Kuu ili kumfungulia kesi  Pinda.

“Tunakusudia kumfungulia kesi Mizengo Pinda kwa kuwa amevunja katiba ya nchi ya usawa mbele ya sheria ambayo ni ibara ya 13 (1),” amesema mkurugenzi huyo.

Mkurugenzi huyo amesema kwamba walitegemea Pinda angefuta kauli yake baada ya kuitoa bungeni lakini badala yake imekuwa kama aliwabariki polisi waendelee kuwapiga raia.

Post a Comment

أحدث أقدم