
Harakati za jeshi dhidi ya Boko Haram
Takriban watu 35 wameuawa katika
mashambulizi matatu yaliyofanywa na wapiganaji wa kiisilamu nchini
Nigeria, kwa mujibu wa maafisa wakuu wa serikali.
Taarifa kutoka kwa jeshi, zinasema kuwa
wapiganaji 32, wanajeshi wawili na polisi walifariki kwenye mashambulizi
hayo, yaliyofanywa dhidi ya kituo cha polisi na dhidi ya kambi ya jeshi
siku ya Jumapili.Kundi hilo lilianza harakati zake mwaka 2009 za kutaka kuligeuza eneo zima la Kaskazini mwa Nigeria kuwa chini ya sheria za kiisilamu.
Zaidi ya watu 2,000 wameuawa tangu kundi hilo kuanza harakati zake.
Mashambulizi hayo mawili katika jimbo la Borno yalifanyika siku ya Jumapili, lakini taarifa za mashambulizi hayo ndizo zimejitokeza tu.
Mawasiliano katika eneo hilo yametatizika tangu sheria ya hali ya hatari kutangazwa .
'Wanajeshi hata hivyo walifanikiwa kuwafurusha wapiganaji wa kiisilamu wa Boko Haram, walionuia kufanya mashambulizi dhidi ya kambi ya jeshi eneo la Bama... Tarehe 4 mwezi Agosti.
Jeshi pia lilisema kuwa kambi ya jeshi mjini Malam Fatori lilishambuliwa na hivyo kusababisha ufyatulianaji wa risasi.
Hata hivyo Boko Haram haijatoa tamko lolote kuhusu mashambulizi hayo.
- BBC
إرسال تعليق