~MBEGU ZA MABOGA: ZINA UWEZO WA KUKUEPUSHA NA MAGONJWA 10 HATARI~~~
A/Alleykum;
ZIKIWA zimesheheni protini na madini kadhaa kama vile chuma, kopa,
maginizia, manganizi na zinki, mbegu za maboga zinakuwa mbegu bora na
muhimu kutafuna kila wakati kama wewe ni mpenzi wa kutafuna-tafuna.
Imethibitika pasipo na shaka kuwa mbegu za maboga zina faida lukuki
kiafya na zina uwezo wa kukuepusha na magonjwa hatari zaidi ya 10:
UGONJWA WA MOYO:
Mbegu za maboga zina kiasi kingi cha madini aina ya maginizia
(magnesium) ambayo huboresha utendaji kazi wa viungo vya mwili.
Huimarisha usukumaji wa damu kwenye moyo, huimarisha ukuaji wa mifupa
na meno, huifanya mishipa ya damu kupitisha damu kwa urahisi na hufanya
upatikanaji wa haja kubwa kuwa laini.
KINGA YA MWILI:
Mbegu
za maboga pia zina kiasi kingi cha madini ya Zinki (Zinc). Madini haya
yana faida nyingi mwilini, ikiwemo kuimarisha kinga ya mwili, kuboresha
ukuaji na uundaji wa chembechembe hai za mwili, kuboresha usingizi,
kuboresha ladha mdomoni na harufu, huboresha afya ya macho na ngozi,
hurekebisha sukari na huboresha nguvu za kiume pia.
Upungufu wa
madini ya ‘Zinc’ mwilini una uhusiano mkubwa sana na matatizo ya kuzaa
watoto njiti, kuota chunusi nyingi mwilini, watoto kuwa na uwezo mdogo
darasani kimasomo na matatizo mengine mengi ya kimwili na kiakili.
MAFUTA YA OMEGA -3:
Omega-3 ni moja kati ya mafuta muhimu sana mwilini. Jamii ya karanga
pamoja na mbegu za maboga ni miongoni mwa mbegu zenye kiasi kingi cha
mafuta aina hii. Hivyo ulaji wa mbegu za maboga utakuwezesha kupata
kirutubisho hiki muhimu katika mwili wako na kukupa faida za mafuta haya
ambazo ni nyingi.
KIBOFU CHA MKOJO:
Tangu enzi za mababu
zetu, mbegu za maboga zimetumika kuimarisha afya ya wanaume kutokana na
kuwa na kiasi kingi sana cha madini aina ya Zinc ambayo ni muhimu sana
kwa afya ya kibofu cha mkojo. Mbegu za maboga pamoja na mafuta yake,
yote kwa pamoja hutoa kinga kwenye kibofu kupatwa na matatizo ya kiafya,
yakiwemo yale ya saratani ya kibofu.
KINGA DHIDI YA SARATANI:
Imethibitika kwamba watu ambao hula mlo wenye kiasi kingi cha mbegu za
maboga wamegundulika kuwa na hatari ndogo sana ya kupatwa na saratani za
tumbo, matiti, mapafu na kibofu.
UGONJWA WA KISUKARI:
Utafiti uliofanywa kwa kuwalisha wanyama mbegu za maboga, umeonesha kuwa
ulaji wa mbegu za maboga, husaidia kurekebisha kiwango cha ‘Insulin’
mwilini na hivyo kumuepusha mtu kupatwa na ugonjwa wa kisukari.
MATATIZO YA UKOMO WA HEDHI:
Mara nyingi kina mama watu wazima ambao wamefikia ukomo wa hedhi,
hupatwa na matatizo mbalimbali yanayosababishwa na hali hiyo. Hata hivyo
utafiti umeonesha kuwa mbegu za maboga zina uwezo wa kurekebisha hali
hiyo na kuondoa kabisa matatizo ya kiafya yatokanayo na ukomo wa hedhi.
AFYA YA MOYO NA MAINI:
Mbegu za maboga, ambazo zina kiasi kingi cha mafuta mazuri, kamba lishe
na virutubisho vinavyoimarisha kinga ya mwili (antioxidants),
zimeonekana kuwa bora pia kwa afya ya moyo na ini, huweza kumpatia mlaji
kinga dhidi ya matatizo ya kiafya katika moyo na ini.
DAWA YA USINGIZI:
Mbegu za maboga zimegundulika pia kuwa na kirutubisho kinachozalisha
‘homoni’ za usingizi. Ulaji wa mbegu za maboga saa chache kabla ya
kupanda kitandani, hasa ukila pamoja na tunda lolote, kunasaidia kupata
usingizi mzuri na tulivu.
DAWA YA UVIMBE:
Tafiti kadhaa
zimeonesha kuwa mbegu za maboga zina mafuta yenye uwezo wa kutoa kinga
dhidi ya magonjwa ya uvimbe (inflamatory diseases) sawa na dawa aina ya
‘indomethacin’, lakini mbegu hizi hazina madhara kama ilivyo kwa hiyo
dawa.
JINSI YA KULA MBEGU ZA MABOGA
Ili kupata faida zake
zote, zikiwemo zile za mafuta yake, inashauriwa kula mbegu hizo zikiwa
kavu, bila kuzikaanga. Hakikisha pia unapata mbegu zilizohifadhiwa
vizuri ambazo hazijaoza wala kuwa na fangasi. Iwapo utapenda kuzikaanga,
basi hakikisha unazikaanga kwa muda usiozidi dakika 15, unaweza pia
kuongeza chumvi kidogo kupata ladha, lakini za kukaanga zitakuwa hazina
mafuta mengi kama zile kavu.
...........Wabillahy towfiq...............
A/Alleykum;
ZIKIWA zimesheheni protini na madini kadhaa kama vile chuma, kopa, maginizia, manganizi na zinki, mbegu za maboga zinakuwa mbegu bora na muhimu kutafuna kila wakati kama wewe ni mpenzi wa kutafuna-tafuna. Imethibitika pasipo na shaka kuwa mbegu za maboga zina faida lukuki kiafya na zina uwezo wa kukuepusha na magonjwa hatari zaidi ya 10:
UGONJWA WA MOYO:
Mbegu za maboga zina kiasi kingi cha madini aina ya maginizia (magnesium) ambayo huboresha utendaji kazi wa viungo vya mwili. Huimarisha usukumaji wa damu kwenye moyo, huimarisha ukuaji wa mifupa na meno, huifanya mishipa ya damu kupitisha damu kwa urahisi na hufanya upatikanaji wa haja kubwa kuwa laini.
KINGA YA MWILI:
Mbegu za maboga pia zina kiasi kingi cha madini ya Zinki (Zinc). Madini haya yana faida nyingi mwilini, ikiwemo kuimarisha kinga ya mwili, kuboresha ukuaji na uundaji wa chembechembe hai za mwili, kuboresha usingizi, kuboresha ladha mdomoni na harufu, huboresha afya ya macho na ngozi, hurekebisha sukari na huboresha nguvu za kiume pia.
Upungufu wa madini ya ‘Zinc’ mwilini una uhusiano mkubwa sana na matatizo ya kuzaa watoto njiti, kuota chunusi nyingi mwilini, watoto kuwa na uwezo mdogo darasani kimasomo na matatizo mengine mengi ya kimwili na kiakili.
MAFUTA YA OMEGA -3:
Omega-3 ni moja kati ya mafuta muhimu sana mwilini. Jamii ya karanga pamoja na mbegu za maboga ni miongoni mwa mbegu zenye kiasi kingi cha mafuta aina hii. Hivyo ulaji wa mbegu za maboga utakuwezesha kupata kirutubisho hiki muhimu katika mwili wako na kukupa faida za mafuta haya ambazo ni nyingi.
KIBOFU CHA MKOJO:
Tangu enzi za mababu zetu, mbegu za maboga zimetumika kuimarisha afya ya wanaume kutokana na kuwa na kiasi kingi sana cha madini aina ya Zinc ambayo ni muhimu sana kwa afya ya kibofu cha mkojo. Mbegu za maboga pamoja na mafuta yake, yote kwa pamoja hutoa kinga kwenye kibofu kupatwa na matatizo ya kiafya, yakiwemo yale ya saratani ya kibofu.
KINGA DHIDI YA SARATANI:
Imethibitika kwamba watu ambao hula mlo wenye kiasi kingi cha mbegu za maboga wamegundulika kuwa na hatari ndogo sana ya kupatwa na saratani za tumbo, matiti, mapafu na kibofu.
UGONJWA WA KISUKARI:
Utafiti uliofanywa kwa kuwalisha wanyama mbegu za maboga, umeonesha kuwa ulaji wa mbegu za maboga, husaidia kurekebisha kiwango cha ‘Insulin’ mwilini na hivyo kumuepusha mtu kupatwa na ugonjwa wa kisukari.
MATATIZO YA UKOMO WA HEDHI:
Mara nyingi kina mama watu wazima ambao wamefikia ukomo wa hedhi, hupatwa na matatizo mbalimbali yanayosababishwa na hali hiyo. Hata hivyo utafiti umeonesha kuwa mbegu za maboga zina uwezo wa kurekebisha hali hiyo na kuondoa kabisa matatizo ya kiafya yatokanayo na ukomo wa hedhi.
AFYA YA MOYO NA MAINI:
Mbegu za maboga, ambazo zina kiasi kingi cha mafuta mazuri, kamba lishe na virutubisho vinavyoimarisha kinga ya mwili (antioxidants), zimeonekana kuwa bora pia kwa afya ya moyo na ini, huweza kumpatia mlaji kinga dhidi ya matatizo ya kiafya katika moyo na ini.
DAWA YA USINGIZI:
Mbegu za maboga zimegundulika pia kuwa na kirutubisho kinachozalisha ‘homoni’ za usingizi. Ulaji wa mbegu za maboga saa chache kabla ya kupanda kitandani, hasa ukila pamoja na tunda lolote, kunasaidia kupata usingizi mzuri na tulivu.
DAWA YA UVIMBE:
Tafiti kadhaa zimeonesha kuwa mbegu za maboga zina mafuta yenye uwezo wa kutoa kinga dhidi ya magonjwa ya uvimbe (inflamatory diseases) sawa na dawa aina ya ‘indomethacin’, lakini mbegu hizi hazina madhara kama ilivyo kwa hiyo dawa.
JINSI YA KULA MBEGU ZA MABOGA
Ili kupata faida zake zote, zikiwemo zile za mafuta yake, inashauriwa kula mbegu hizo zikiwa kavu, bila kuzikaanga. Hakikisha pia unapata mbegu zilizohifadhiwa vizuri ambazo hazijaoza wala kuwa na fangasi. Iwapo utapenda kuzikaanga, basi hakikisha unazikaanga kwa muda usiozidi dakika 15, unaweza pia kuongeza chumvi kidogo kupata ladha, lakini za kukaanga zitakuwa hazina mafuta mengi kama zile kavu.
...........Wabillahy towfiq...............
Post a Comment